Mgombea udiwani monduli mjini kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Izak Joseph
akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Monduli juzi katika viwanja vya
soko la alhamis wakati akizindua rasmi kampeni za mgombea
huyo.
************
Wagombea Udiwani na Ubunge jimbo la Monduli kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wametaja sekta ya elimu kuwa moja
ya vipaumbele watakapofanikiwa kushinda uchaguzi mkuu ujao.
Akihutubia mkutano wa kampeni mjini Monduli juzi, mgombea
ubunge kupitia Chadema Julius Kalanga alisema elimu ni msingi wa
maendeleo katika sekta zote kwa sababu ndio huzalisha wataalam na
watendaji katika miradi yote ya maendeleo.
"Aliyekuwa mbunge wa Monduli, Mheshimiwa Edward Lowassa
amefanya makubwa katika sekta ya elimu, siyo tu Monduli, bali eneo lote
la jamii ya wafugaji wa Kimaasai ambao kihistoria walionekana kubaki
nyuma kieleimu. Nitaendeleza yote," alisema Kalanga
Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni afya, miundombinu,
mawasiliano, uwezeshaji na uimarishaji wa miradi midogo midogo kupitia
vikundi vya ujasiriamali pamoja na uhamasiahaji wa umma kushiriki
harakati za maendeleo kwa kupanga, kuchangia, kitekeleza na kusimamia
miradi katika maeneo yao.
Kwa upande wake, mgombea udiwani kata ya Monduli mjini,
Isack Joseph "Kadogoo" anayetetea nafasi yake aliahidi kuendelea
kuwalipia ada wanafunzi wote watakaofauli kuendelea na elimu ya
sekondari ndani yakata yake, lakini wazazi au walezi hawana uwezo wa
kugharamia elimu yao.
"Tangu niwe diwani mwaka 2010 hadi sasa nimeshawalipia
zaidi ya wanafunzi 75 wanaosoma shule mbalimbali za sekondari ndani na
nje ya wilaya ya Monduli. Nitaendelea kufanya hivyo," alisema Joseph
Alisema awali alikuwa akitumia fedha zake binafsi kabla ya
kuingiza programu hiyo katika mipango ya matumizi ya fedha za maendeleo
ya kata ili kuwezesha mradi wa ada kwa wanafunzi kuwa endelevu kwa kila
diwani atakayefuata badala ya kubaki jambo lake binafsi.
0 comments:
Post a Comment