Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki, Celine
Kombani (56),amefariki dunia hii leo nchini India .
Kombani alipitishwa na Chama
cha Mapinduzi kutetea jimbo lake la Ulanga Mashariki na alipita bila kupingwa
katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza
kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo
Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa
mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la
Ulanga.
**********
Anaandika Father Kidevu
TUJIKUMBUSHE KUHUSU JIMBO LA ULANGA MASHARIKI
JIMBO la Ulanga kabla ya
kugawanywa na kutoa majimbo mawili ya Ulanga Magharibi na Ulanga Mashariki
lilipata kuongozwa na Mbunge wa zamani wa Ulanga, Nazar Nyoni aliyepata kuwa
Naibu Waziri wa Elimu kati ya mwaka 1975 hadi 1980.
Jimbo la Ulanga liligawanywa
na Ulanga Mashariki aliingia Marehemu Guntram Amani Mkolokoti Itatiro,
aliyefariki bado akiwa Mbunge 1999 na nafasi yake kushikwa na Kapteni
Mstaafu Theodos James Kasapira ambaye alifariki ghafla akiwa Bungeni Mjini
Dodoma akihudhuria kikao cha Bunge la Bajeti Mkutano wa 16 katika Kikao cha 32
kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe Julai 22, 2004.
kisha kuingia Celine Ompeshi
Kombani ambae nae amefariki akiwa madarakani na tayari kutetea nafasi yake
katika uchaguzi Mkuu unaotaraji kufanyika Oktoba 25, 2015.
ELIMU YA DARASANI
Mamam Kombani alipata elimu
yake ya msingi katika Shule ya Msingi Kwiro 1968-1975 na baadae kuchaguliwa
kujiunga na Sekondari ya Wasichana Kilakala 1975-1978 na kuendelea na kidato
cha tano na sita Sekondari ya Wasichana Tabora 1979-1981.
Mwaka 1982 Celine Kombani
alijuunga na Taasisi ya Uongozi na Maendeleo Mzumbe (IDM) na kuchukua Shahada
ya kwanza ya uongozi na Utawala (B.A) aliyohitimu mwaka 1985.
Mwaka 1994 Celine Kombani
alirejea tena IDM Mzumbe ambacho hivi sasa ni Chuo Kikuu Mzumbe (MU) na kusoma
Shahada ya Uzamili ya Uongozi na Utawala aliyohitimu 1995.
Pia amepata kuhudhuria semina,
Warsha na Makongamano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ambayo yalizidi
kumuimarisha katika utendaji kazi wake.
UONGOZI
Celine baada ya kuhitimu
Shahada ya kwanza ya Uongozi na Maendeleo IDM Mzumbe, aliajiriwa Ofisi ya
Halmashauri ya Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro alipodumu hadi mwaka 1992 kabla ya
mwaka 1994 kuajiriwa kiwanda cha Maturubai Morogoro kama Meneja ambako napo
alidumu kwa mwaka mmoja na kupata ajira nyingine 1995 Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine (SUA) mkoani Morogoro kama Afisa Tawala Mwandamizi, kazi
aliyoifanya hadi 2005.
Celene, aliamua kuingia katika
siasa na kuwania ubunge katika Jimbo la Ulanga Mashariki katika Uchaguzi
uliofanyika Oktoba 25 2005, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Marehemu Capt
(Mstaafu), Theodos James Kasapira, aliyefariki ghafla akiwa Bungeni Mjini
Dodoma akihudhuria kikao cha Bunge la Bajeti Mkutano wa 16 katika Mkutano wa 32
kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe Julai 22, 2004.
Baada ya jkurithi mikoba hiyo
ya Capt Kasapira, 2006 alichaguliwa kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) alidumu hadi 2008 baraza la
mawaziri lilipovunjwa na Edward Lowassa kujiuzulu na Waziri Mkuu wa sasa
Mizengo Pinda kuingia madarakani alipanda na Kuwa Waziri kamili wa TAMISEMI.
Mwaka 2010 aliteuliwa kuwa
Waziri wa Katiba na Sheria kabla ya Kuhamishiwa tena Ofisi ya Rais na kuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Utumishi) hadi
mauti yanamfika.
SIASA
Kwa upande wa Siasa mwaka
1987-1992 alikuwa ni mwanachama wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi
(UWT) na alikuwa mjumbe wa Kamati Maalum ya Chama hicho Kilosa.
Aidha Kombani aliwahi kuwa
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya
Morogoro hii ikiwa ni 2002 hadi 2005.
Omg,,,RIP Celina..
ReplyDelete