Mfanyaakzi
wa Airtel, (kulia), akijaza fomu ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari
(Wote Scheme), wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa ufunguzi wa wiki ya
Wafanyakazi wa Airtel, makao makuu ya kampuni hiyo ya simu za mikononi, jijini
Dar es Salaam, Septemba 26, 2015.
Wafanyakazi
wa Airtel, wakipatiwa maelezo juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na PPF, wkati
wa wiki ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ya simu makao makuu ya Airtel, Morocco
jijini Dar es Salaam, Septemba 26, 2015.
Meneja
Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, (kulia), akizungumza jambo na Meneja Uhusiano
wa Airtel, Jackson Mbando, wakatyi wa ufunguzi wa wiki ya Wafanyakazi wa Airtel
NA
K-VIS MEDIA
MFUKO
wa Pensheni wa PPF, umevuna wanachama wapya kadhaa kwenye Wiki ya Wafanyakazi
wa kampuni ya simu za mikononi, Airtel, iliyoanza leo Septemba 26, 2015 pale
makao makuu ya Airtel, Morocco jijini Dar es Salaam.
Akizungnumza
na waandishi wa habari wakati wa utoaji huduma kwa wafanyakazi hao, Meneja
Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, amesema, Airtel ni moja ya “Akaunti’ kubwa za
PPF, kwa maana ya Mfuko kuwa na idadi kubwa ya wanachama kutoka kampuni hiyo,
hivyo wameitumia fursa hiyo kutoa elimu ya huduma mbalimbali zitolewazo na
Mfuko.
“Pamoja
na kusajili wanachama wapya chini ya Mpangop wa Wote Scheme, yaani ucnangiaji
wa hiari, pia tumewaeleza wanachama wetu kuhusu mafao mapya yatolewayo na Mfuko
kama fao la Uzazi.” Alifafanyua Ngowi.
Meneja
Msoko huo wa PPF pia alisema, Wanachama wa PPF kupitia mpango huo wa wote
scheme, wanaweza kujiunga na bima ya afya ya NHIF, ambapo PPF inakuwa mdhamini
wa wanachama wake kupitia mpango huo wa uchangiaji wa hiari (Wote Scheme).
Afisa
Uwekezaji Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo, (kulia),
akimsikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, wakati wa utoaji huduma kwenye wiki ya
wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel, makao makuu ya kampuni
hiyo jijini Dar es Salaam
Afisa
wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam, Saluna Aziz Ally, (kushoto), akimeuelekeza Mwanachama wa Mfuko huo
jinsi ya kupata taarifa za michango yake kupitia simu ya mkunoni, huduma
ijulikanayo kama “PPF Taarifa), wakati wa ufunghuzi wa wiki ya wafanyakazi wa
Airtel, iliyoanza leo Sptemba 26, 2015 pale makao makuu ya kampuni hiyo ya simu
za mikononi, Morocco jijini Dar es Salaam
Mwanachama
mpya wa PPF akijaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (Wote
Scheme), wakati wa ufunguzi wa wiki ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za
mikononi, Airetel, jijini Dar es Salaam
Afisa
Operesheni wa Kanda wa Mfuko wa Pensehni wa PPF, Upendo Singinika, (kulia),
akimpatia zawadi mwanachama wa Mfuko huo baada ya kupatiwa maelezo ya huduma
mbaklimbali zitolewazo na Mfuko huo, kwenye ufunguzi wa wiki ya wafanyakazi wa
Airtel makao makuu ya kampuni hiyo ya simu za mikononi jijini Dar es Salaam
Afisa
Masoko wa PPF, Francis Kihinga, akimpatia maelezo ya kina mwanachama wa PPF
Abib
Kibiki, (kushoto), Afisa Masoko wa PPF, akimpatia maelezo Mfanyakazi huyu wa
Airtel, wakati wa wiki ya wafanyakazi wa Airtel
Afisa
operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Upendo Singinika, (kulia), akishauriana
jambo na Mtaalamu wa mifumo ya Computer wa Mfuko huo, Gideon Mwashihongo,
wakati wa wiki ya wafanyakazi wa Aiortel,ambapo PPF ilitumia fursa hiyo
kusajili wanachama wapya chini ya mpango wa Wote Scheme
Mfanyaakzi wa Airtel, (kulia), akitumia simu yake ya mkononi, kupata taarifa za michango yake ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, kupitia huduma ya PPF Taarifa
0 comments:
Post a Comment