Nafasi Ya Matangazo

September 15, 2015

IMG_8938
Mwenyekiti wa National Governance Internet Forum ambaye pia ni Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya akiwakaribisha wadau wa mitandao na watumiaji wa intaneti kwenye jukwaa hilo kabla ya kumkaribisha mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA kufungua rasmi jukwaa hilo.. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tanzania Education and Research Network (TERNET), Amos Nungu na Kushoto ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akifuatiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Sunday Richard. 
IMG_9056
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Sunday Richard akifungua rasmi Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya mtandao (NIGF) lililoandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kufanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano COSTECH jijini Dar. Kushoto ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph aliyemwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO na kulia Mwenyekiti wa National Governance Internet Forum, Kenneth Simbaya.
IMG_9206 
IMG_9182  
Sehemu ya washiriki waliohudhuria jukwaa hilo wakifuatilia "presentation" iliyokuwa ikitolewa na Mtaalamu kutoka TCRA Dk. Emmanuel Manasseh (hayupo pichani). PICHA ZAIDI >>>FK MATUKIO
Posted by MROKI On Tuesday, September 15, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo