Nafasi Ya Matangazo

September 15, 2015

 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,akiwahutubia Wananchi wa Tabora jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa  Ali Hassan Mwinyi.Dkt Magufuli alisema kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.

 Sehemu ya umati wa watu waliokuwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
  Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tabora waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia anataka kujenga Tanzania mpya yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
 Mmoja wa Makada walioko kwenye timu ya uhamasishaji wa kampeni za CCM,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa Tabora kwenye mkutano wa kampeni za Urais ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo.
PICHA ZAIDI >>>FK MATUKIO
Posted by MROKI On Tuesday, September 15, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo