Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Prof. Sifuni Mchome (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Mamlaka ya Elimu (TEA) zilipotialiana saini mkataba wa makubaliano ambapo TEA itaipatia TET Mkopo wa Sh Bilioni 3 kwaajili ya kuandaa mitaala na kuchapisha vitabu vitakavyotumiwa na
wanafunzi shule za msingi nchini kuanzia darasa la tatu hadi la sita. Prof Mchome, amewataka TET kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo
kwa weledi ili kuweza kusaidia mabadiliko ambayo yatachangia kuwa na elimu
inayokidhi viwango vya kimataifa.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Joel Laurent na Kaimu Mkurugenzi wa TET, Dk
Leonard Akwilapo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),
Dk Leonard Akwilapo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya
Elimu Tanzania (TEA), Joel Lauren (kulia) wakitiliana
saini hati za makubalino ya mkopo wa Sh Bilioni 3 ambazo TEA itaipatioa TET. Katikati
ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),
Dk Leonard Akwilapo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya
Elimu Tanzania (TEA), Joel Lauren (kulia) wakionesha
hati za makubalino ya mkopo wa Sh Bilioni 3 ambazo TEA itaipatioa TET baada ya
kutiliana saini jana mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Prof. Sifuni Mchome.Picha: Father Kidevu Blog.
Picha ya pamoja ya Wakurugenzi wa TEA, TET, Katibu Mkuu pamoja na watumishi wao.
**************
Na Father Kidevu Blog
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imeipatia mkopo
wa shilingi Bilioni 3 Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) katika makubaliano
yaliyofikiwa leo Septemba 30, 2015 jijini Dar es Salaam.
Makubaliano hayo yalifikiwa mbele ya Katibu Mkuu
Wizara ya Eklimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome ambapo TET itatumia
fedha hizo katika kuandaa mitaala na kuchapisha vitabu vitakavyotumiwa na
wanafunzi shule za msingi nchini kuanzia darasa la tatu hadi la sita.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Joel Laurent amesema
mkopo huo nafuu utakaolipwa katika kipindi cha miaka sita, umetolewa katika
kutekeleza sera mpya ya elimu ya mwaka 2014.
“Mamlaka kwa kuzingatia Sera mpya ya Elimu ya
mwaka 2014, imeridhia maombi ya mkopo ili kuhakikisha uwepo wa mitaala, muhtasari
na vitabu vya kiada kwa darasa la tatu hadi la sita vinavyoendana na mahitaji
na wakati,”alisema Laurent.
Utaratibu huo utaiwezesha TET kuandaa vitabu vya
kiada kwa hatua ya kwanza ya elimu msingi, kutafanya uwepo wa mitaala
inayoendana na kuwa kuboresha mfumo wa upatikanaji wa vitabu sahihi kulingana
na mitaala nchi nzima kupitia TET hivyo Sasa nchi itakuwa na kuwa na kitabu
kimoja cha kiada kwa shule nzima tofauti na ilivyo sasa kila shule zinavitabu
vyake vya kufundishia.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk
Leonard Akwilapo alisema mkopo huo watautumia kufanya utafiti na kubaini
mahitaji ya maboresho kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwamo
wanafunzi, walimu, wazazi na waajiri na kuandaa mitaala ya Elimu ya awali na
Elimu ya Msingi kuanzia darasa la tatu hadi sita na kuandika vitabu vya kiada.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Prof. Sifuni Mchome aliwataka TET kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo
kwa weledi ili kuweza kusaidia mabadiliko ambayo yatachangia kuwa na elimu
inayokidhi viwango vya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment