UZUSHI KUHUSU AFYA YA MKUU WA
MAJES KUMEKUWAPO UVUMI WENYE
KUUPOTOSHA UMMA KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NCHINI AMENUSURIKA KIFO BAADA YA
KUWEKEWA SUMU KATIKA CHAKULA NA HIVI SASA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN
ILIYOPO NAIROBI, NCHINI KENYA, HUKU WENGINE WAKIDAI KUWA YUKO NCHINI INDIA KWA
MATIBABU.
TAARIFA HIZO NI UONGO WENYE
KILA DALILI YA KUTENGENEZWA KWA LENGO LA KUWATIA HOFU WATANZANIA JUU YA USALAMA
WA KIONGOZI HUYU WA JUU WA MAJESHI YETU.
UKWELI NI KUWA MKUU WA MAJESHI
YA ULINZI, JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE NI BUKHERI WA AFYA NA HAYUPO NCHINI KENYA
WALA INDIA KAMA ILIVYOENEZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA VYOMBO VYA HABARI.
TUNAPENDA KUWATOA HOFU
WANANCHI KUWA TAARIFA HIZO NI UZUSHI MTUPU KWANI JENERALI MWAMUNYANGE ALIONDOKA
NCHINI TAREHE 22 SEPTEMBA 2015, SAA 10.45 JIONI KWA NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE
LA EMIRATES KUELEKEA ROME, ITALIA KWA ZIARA YA KIKAZI KUFUATIA MWALIKO WA MKUU
WA MAJESHI WA JAMHURI YA ITALIA, JENERALI CLAUDIO GRAZIANO. TUNAPENDA
KUWAHAKIKISHIA WANANCHI KUWA JENERALI MWAMUNYANGE PAMOJA NA UJUMBE WAKE
WANAENDELEA NA ZIARA HIYO KAMA ILIVYOPANGWA NA AMESIKITISHWA NA UVUMI HUO.
WIZARA YA ULINZI YA JESHI LA
KUJENGA TAIFA IMESIKITISHWA NA TABIA HII YA UZUSHI INAYOPINGANA NA WELEDI NA
KANUNI ZA UANDISHI KATIKA TASNIA YA HABARI. NI DHAHIRI TABIA HII INAIDHALILISHA
TASNIA YA HABARI NA WANAHABARI WANAOZINGATIA WELEDI NCHINI. TUNAPENDA KUCHUKUA
FURSA HII KUKEMEA TAARIFA ZA AINA HII ZISIZOKUWA NA TIJA KWA TAIFA LETU NA
ZILIZOLENGA KUWASUMBUA NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA WATUMISHI WENYE MAPENZI YA
DHATI NA JENERALI MWAMUNYANGE.
TUNAWAASA WANAHABARI
KUTOZITUMIA VIBAYA KALAMU ZAO NA UHURU WALIONAO KWA NAMNA YOYOTE ISIYOKUWA NA
TIJA KWA TAIFA LETU. AIDHA, WIZARA NA TAASISI ZAKE WAKATI WOTE ZIMEKUWA TAYARI
KUTHIBITISHA JAMBO LOLOTE AU KUTOA UFAFANUZI PALE ULIPOHITAJIKA. INASTAAJABISHA
KUONA WALIOANZISHA UZUSHI HUO NA KUUENEZA HAWAKUWA TAYARI KUOMBA UTHIBITISHO WA
NAMNA YOYOTE. JAMBO HILI LINATIA SHAKA JUU YA NIA YA MTU AU KIKUNDI
KILICHOANZISHA UVUMI HUO.
WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA
KUJENGA TAIFA NA TAASISI ZAKE ZITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO WA DHATI KWA
WANAHABARI WENYE NIA YA DHATI YA KUJENGA NA KUILETEA SIFA TASNIA YA HABARI KWA
KUZINGATIA WELEDI. UHURU WA VYOMBO VYA HABARI UWE NI UHURU WENYE KUZINGATIA
WAJIBU ULIOBAINISHWA KATIKA MAADILI NA KANUNI ZA UANDISHI WA HABARI.
MWISHO, TUNAWATAKA
WALIOANZISHA UZUSHI HUO KUMUOMBA RADHI JENERALI MWAMUNYANGE KAMA ISHARA YA
USTAARABU NA KUTAMBUA KUTELEZA KWAO. KUTOFANYA HIVYO ITATAFSIRIKA KUWA NI
KUKIRI KUWA KUENEZA UZUSHI HUO HAIKUWA KUTELEZA, BALI ILIKUSUDIWA KWA DHAMIRA
FULANI, NA HIVYO KUSHAWISHI HATUA ZAIDI KUCHUKULIWA.
JESHI NA WIZARA ZITAENDELEA
KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA HUSIKA KUWABAINI WATU WALIOHUSIKA KUUTUMIA VIBAYA UHURU
WA HABARI NA HIVYO KUUPOTOSHA UMMA NA KULETA USUMBUFU KWA FAMILIA YA JENERALI
MWAMUNYANGE, JESHI NA TAIFA KWA UJUMLA.
Luteni Kanali Juma Nkangaa
Sipe,
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa.
Mob: 0756 448787/ 0682 448787.
0 comments:
Post a Comment