Mwenyekiti wa
Chama cha Wakulima Kanda ya Kaskazini(Taso)Arthur Kitonga akisoma
taarifa ya Taso inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro,Manyara na Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa
Manyara ambao ni wanachama wa Taso Kanda ya Kaskazini,Mh Joel Bendera
akisistiza jambo kwenye mkutano wa ufunguzi uliofanyika kwenye viwanja
ya Nanaenane Njiro jijini Arusha,anayesikiliza kwa makini ni Mkuu wa
mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda(wa pili kushoto).
Meneja wa Shama la
Mbegu la Serikali mkoa wa Arusha,Zawadiel Mrinji akionesha mfuko
ulitengenezwa maalumu kwa lengo la kudhibiti wadudu waharibifu baada ya
mavuno ili kumwezesha mkulima kunufaika na mazao yake.
Meneja wa Shama
la Mbegu la Serikali(ASA) mkoa wa Arusha,Zawadiel Mrinji akizungumzia
umuhimu wa zao la Ngano linalostawi kwa wingi wilaya ya Monduli na
Hanang .
Viongozi wa
serikali wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda(wa tatu
kulia)wakikagua bustani ya JKT ambayo imekua kivutio kwa wananchi
wanaotembelea maonesho ya Nanenane Njiro mkoani Arusha.
Viongozi wa
serikali wakikagua bustani ya JKT ambayo imekua kivutio kwa wananchi
wanaotembelea maonesho ya Nanenane Njiro mkoani Arusha.
Bustani ya taasisi ya Utafiti wa Kahawa(Tacri)hutembelewa na wakulima kujifunza namna bora ya kilimo cha Buni nchini.
Wananchi wakipata maelezo kutoka kwenye banda la Sementi la Simba Cement .
Baadhi ya
wafanyakazi wa Benki Kuu(Arusha) ambao wanashiriki kwenye maonesho hayo
wakijumuika na wananchi kusikiliza hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha
,Felix Ntibenda.
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)Oljoro mkoa wa Arusha wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi.
Wanafunzi wakiwa kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kujifunza mambo mbalimbali yanatolewa na Chuo hicho.
Kikundi cha burudani kutoka JKT Oljoro wakionesha ufundi wao wa ngoma kutoka Pemba. Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment