MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa, (kulia),
akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania 2015, za Tume hya Taifa ya Uchaguzi, (NEC),
kutoka kwa afisa mwandamizi wa tume hiyo, makao makuu ya NEC, jijini Dar
es Salaam leo asubuhi Jumamosi Agosti 1, 2015. Dovutwa amekuwa mgombea
wa kwanza kuchukua fomu hizo na kazi iliyo mbele yake ni kutafuta
wadhamini 200 ambao ni raia wa Tanzania wenye shahada za kujiandikisha
kupiga kura kwenye uchaguzi huo. Dovutwa alifuatana na mgombea mwenza
wake, Hamad Mohammed UIbrahim na wanachama wachache wa chama hicho
Mgombea kiti cha Urais kupitia TLP, Maxmillian Lyimo, (kulia), akipokea
mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti hicho za Tume ya Taifa ya
Uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment