Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji wakiwasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015.
Umati wa wakazi wa Jijini Dar es salaam, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye viwanja vya Jangwani kuwalaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015.
Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakiwashangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akimkabidhi, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, Kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa mwaka 2015/2020 mara baada ya kuizindua, leo Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakionyesha vitabu cha Ilani ya Uchaguzi mara baada ya kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe.
Viongozi wa Vyama mbali mbali vinavyounda UKAWA wakionyesha Ilani hiyo mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam, leo Agosti 29, 2015.
Picha zaidi Boyfa FK MATUKIO
0 comments:
Post a Comment