Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limesogezwa mbele kufungwa kwa dirisha la
usajili wa wachezaji kwa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
na Ligi Daraja la Pili (SDL) mpaka Agosti 20 mwaka huu.
Awali
dirisha la usajili lilikua lifungwe leo Agosti 6, na usajili mdogo wa ndani
ungefungwa Septemba 5, 2015 lakini sasa usajili wote kwa jumla utafungwa Agosti
20, 2015.
Tarehe
21- 28 Agosti, 2015 ni kipindi cha pingamizi, tarehe 29-30 Agosti 2015, Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapitia na kupitisha usajili.
Dirisha
la uhamisho wa wachezaji wa Kiamataifa (FIFA –TMS) litafungwa tarehe 06 Septemba,
2015 na Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.
TFF
inavitaka vilabu kukamilisha usajili huo katika muda huo uliowekwa, ili
kupunguza usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho,na dirisha
litakapofungwa Agosti 20, litafunguliwa tena wakati wa dirisha dogo mwezi
Novemba 15 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment