Kocha Mkuu mpya wa timu ya taifa
ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa (kushoto) akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni msaidizi wake,
Hemed Morocco.
**************
Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza
kikosi cha wachezaji 29 watakaongia kambini siku ya Jumapili tarehe 9, Agosti
katika hoteli ya Tansoma iliyopoe eneo la Gerezani kwa ajili ya kambi ya wiki
moja ya mazoezi.
Katika
kikosi hicho alichokitangaza cha wachezaji 29, Mkwasa amewajumuisha wachezaji
watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi (Proffesional), ambao baadae watajumuika
kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria mwezi Septemba 2015 nchini Uturuki.
Taifa
Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku kumi jijini Istambul - Uturuki, ambapo
itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla
ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria.
Wachezaji
watakaongia kambini jumapili ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga SC) na Aishi
Manula (Azam FC), walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan
(Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na Abdi Banda (Simba SC).
Walinzi
wa kati; Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub, Kelvin Yondani (Yanga SC),
Viungo wakabaji: Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Viungo
washambuliaji ni Salum Telela (Yanga SC) na Said Ndemla (Simba SC).
Washambuliaji
wa pembeni; Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus
Kaseke, Saimon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano, Farid Musa (Azam FC), huku
washambuliaji wa kati wakiwa ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid
Mandawa (Mwadui FC).
Wachezaji
wa kimataifa waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea
kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samata, Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe – DR Congo), Mrisho Ngasa (Free State - Afrika Kusini) na
Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town –
Uingereza)
0 comments:
Post a Comment