Nafasi Ya Matangazo

August 30, 2015

  Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa nchini Bw. Ammishadai Owusu-Amoah akimkabidhi Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT mfano wa hundi wenye ya dola za kimarekani 100,000 kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda. Nyuma ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassani Mwinyi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bank of Afrika Mwanaidi Majaar.
 Balozi Mwanaidi Majaar,Mwenyekiti wa Bodi Bank of Afrika akihutubia wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo. Balazo anasema BOA wamejizatiti kurudisha kwa jamii wanayoihudumia na harambee ya kutibu watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda ni moja ya mafanikia ya taratibu wao.
 Matembezi ya hisani ya pamoja yaliyoandaliwa na BOA na CCBRT hospitali kutoka Leaders clup mpaka CCBRT kuadhimisha kilele cha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akihutibia na kupongeza kwa dhati juhudi zilizofanya na zinazoendelea kufanywa na  Bank of Africa kwa kujali jamii na kuhusia wadau wengine pia kuiga mfano wa BOA
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akimsalimia mtoto aliyeshiriki katika matembezi hayo.
Matembezi ya hisani  kuadhimisha kilele cha ukusanyaji fedha yakiendelea kueleka hospital ya CCBRT

NA  FRANCIS DANDE

RAIS wa Awamu ya Pili, Ali Hssan Mwinyi, jana aliongoza  matembezi ya hisani ya kilometa tatu kutoka Leaders Club, Kinondoni hadi Hospitali ya CCBRT Msasani kwa ajili ya kuchangia  matibabu ya watoto waliopinda miguu.

Matembezi hayo yaliyodhaminiawa  na Benki ya Afrika - Tanzania, lengo kuu lilikuwa ni kukusanya dola za marekani laki moja kwa madhumuni ya kugharamia watoto wenye miguu iliyopinda nchini kote. Ilikuwa ni kilele cha kampeni ya  ukusanyaji wa dola za Marekani laki moja iliyozinduliwa mwezi Aprili mwaka  huu.
Kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha  CCBRT kutoa matibabu ya gharama nafuu kwa watoto  400 wenye ugonjwa wa kupinda miguu nchini kote,ilikuyabadili  maisha  yao na kuwa  ya kawaida.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo jana,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Benki ya Afrika – Tanzania, Mwanaidi Maajar, alisema: “Benki ya Afrika – Tanzania imedhamiria kurejesha kwa jamii kile  inachopata  kwa kuwa inaendesha  shughuli  zake, kwa kuchangia mahitaji mbalimbali ya jamii husika. Tumeona umhimu wa kuhimiza  usaidizi katika suala hili jema, kwa kuwa  CCBRT inatoahuduma kawa jamii maskini kwa kuondoa vikwazo mbalimbali ili jamii husika iweze  kupata  matibabu,” alisema Mwanaidi .

Aidha , Ofisa Mendaji mkuu wa CCBRT,Erwin Telemans alisisitiza: “ CCBRT inatoa shukrani za pekee kwa  Benki ya Afrika –Tanzania kutokana na ukarimu wao katika kipindi chote  cha kampeni hii. Maisha ya  a mamia ya  watoto wenye ugonjwa wa kupinda miguu watapona kwa uhakika kutokana na matibabu watakayopatiwa na CCBRT, na hatutaweza kuya badili maisha  ya watoto hao bila  kupata msaada kutoka kwa washirika wetu wakarimu kama Benki ya Afrika – Tanzania.”
Posted by MROKI On Sunday, August 30, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo