USIKU
wa kumkia jana Jeshi la Polisi lilipata pigo kubwa kufuatia vifo vya askari
wake 4 na mwingine kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kuvamia kitio Kikuu
cha Polisi Stakishari Ukonga.
Kituo
hiki ni kikubwa kwani ni Kituo Kikuu cha Wilaya ya Kipolisi ya Ukonga, katika
Kanda maalum ya Dar es Salaam ambacho kina wajibika katika mkoa wa Kipolisi
Ilala.
Naandika
hapa huku nikiwa na majonzi na huzuni kubwa kufuatia vifo vya wapendwa wetu
hawa. Pia walikufa raia watatu huku mmoja akihisiwa kushiriki katika tukio hilo
na kuuwawa na wenzake hao.
Hili
la Ukonga Stakishari limetokea wakati bado hatujasahau yaliyotokea katika vituo
vingi vya Polisi kama Newala, Ikwiriri, Kimanzichana na Bukombe ambapo
iliripotiwa jumla ya silaha 41 zimeporwa na baade 32 kupatikana lakini pia
askari zaidi ya 5 kuuwawa.
Tukio
hili la Ukonga Stakishari limetokea ikiwa imepita miezi minne tangu Rais jakaya
Kikwete alipozungumzia wimbo hilo la mashambulizi kwenye vituo vya polisi
nchini.
Rais
Kikwete akihutubia taifa miezi minne iliyopita, alisema kuwa polisi wanachunguza sababu ya uvamizi huo.
Bila shaka na ninaamini kuwa uchunguzi huo ulisha baini sababu ya uvamizi huo.
Lakini
jana tumeshuhudia tena jinamizi hilo la uvamizi na uwaji wa Polisi vituoni nchini
ukianza tena baada ya kimya cha muda mrefu na wananchi tuliamini kudhibitiwa
kwa hali hiyo. Soma Zaidi Hapa
0 comments:
Post a Comment