Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Huawei Technologies Tanzania, Samson Majwala (kushoto) akiwa na Meneja Mkaazi wa Huawei nchini, Zhang Junliang wakionesha simu mpya aina ya Huawei P8 wakati wa uzinduzi wake katika soko la Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Huawei Technologies Tanzania, Samson Majwala akiielezea simu muundo wa simu hiyo Huawei P8.
Meneja
Mkazi anayeshughulikia bidhaa za kampuni ya Huawei Tanzania, Bw. Zhang
Junliang, akitoa taarifa fupi ya simu ya Huawei P8 mbele ya waandishi wa
habari na wageni waalikwa (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Warembo
wakipozi na kuonyesha simu ya Huawei P8 ambayo itaanza kupatikana
katika soko la Tanzania kuanzia leo na itakuwa inauzwa kwa gharama nafuu
ya shillingi 1,100,000 kwa simu inayotumia laini 1 na shillingi
1,200,000/- kwa simu inayotumia laini mbili.
Mpiga
picha wa gazeti la Serikali la Habari Leo, Mroki Mroki almaarufu kama
Father Kidevu (kulia) akithibitisha ubora wa simu ya Huawei P8 wakati wa
hafla fupi ya uzinduzi wa simu hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na
Mauzo wa kampuni ya Huawei Tanzania, Bw.Samson Majwala.
*************
BAADA ya kufanyika uzinduzi mkubwa wa simu ya
Huawei P8 mjini Johannesburg hivi karibuni, kampuni hiyo nguli katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano ya Huawei, leo hii imezindua
simu mpya ya P8 jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa
kampuni hiyo kuleta mapinduzi kwenye nyanja ya mawasiliano ulimwenguni.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu hiyo leo kwa
waandishi wa habari na wageni waalikwa katika hafla iliyofanyika katika hoteli
ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es
Salaam, Mkurungezi wa Masoko na Mauzo wa Huawei Tanzania Bwana Samson Majwala
alisema uundwaji wa simu hiyo umelenga kurahisisha zaidi mahitaji ya teknolojia
ya mawasiliano kwa watumiaji wa simu za kisasa zilizotengenezwa kutosheleza
mahitaji mbalimbali ya wateja mbali na kutumika katika mawasiliano.
Alisema simu hii ya P8 itaanza kupatikana katika
soko la Tanzania kuanzia leo na itakuwa inauzwa kwa gharama nafuu ya shillingi
1,100,000 kwa simu inayotumia laini 1 na shillingi 1,200,000/- kwa simu
inayotumia laini mbili“Na hiyo ndiyo sababu kila mfumo wa simu hii upo kisasa
zaidi kuanzia muonekano wake ambao kiukweli ni ‘bapa’ kurahisisha ushikwaji
wake, rangi zake zenye mvuto sambamba na
kamera yenye uwezo wa hali ya juu yenye kukidhi kiu ya kiubunifu kwa
kila mtumiaji wake,’’ alifafanua.
Kwa mujibu wa Bwana Majwala, simu hiyo ya P8
ambayo inaingia sokoni ikiwa na rangi tofauti nne za dhahabu, nyeusi, fedha na
kijivu imeboreshwa zaidi ikiwemo kwenye mfumo wake wa ‘kutafutwa kwa sauti’,
alisema.
Akizungumzia ubora wa betri ya simu hiyo Bwana
Majwala alisisitiza kwamba mfumo wa simu hiyo imezingatia matumizi ya muda
mrefu kwa mfano mtumiaji anaweza kutumia simu kwa siku nzima bila kuiongezea umeme
huku kwa wale watumiaji wa kawaida anaweza kuitumia kwa siku moja na nusu.
“Mapinduzi mengine kwenye simu hii yanajidhihirisha kwenye mfumo wake wa kamera
ya kupiga picha na kurekodi video
ambavyo vimeboreshwa zaidi hususani katika uchukuaji wa picha.
Sifa nyingine ya pekee katika simu hii mpya ya
P8 ni kuwa na uwezo wa kuongezeka sauti kuwa kubwa kwa kiwango cha asilimia 58
zaidi ya kiwango cha kawaida iwapo mtumiaji anakuwa kwenye sehemu zenye kelele
na kuwa rahisi kwake kuendelea kupata mawasiliano na haina mawimbi endapo mtumiaji
anaitumia kwa kutumia waya maalumu wa kusikilizia simu masikioni au unapotumia
kipaza sauti kimoja cha simu bila kusahau kudumu na chaji ya betri kwa muda
mrefu.
Pia simu hii mpya mbali na kuwa na mambo mengi
ya kisasa na yanayoleta furaha kwa mtumiaji inaouwezo wa kuifadhi kiasi kikubwa
cha kumbukumbu kufikia 16GB au 64GB na ikiunganishwa na interneti inakuwa na kasi ya ajabu katika
kupakua data uwezo wake ukiwa zaidi ya mara tatu ya uwezo wa simu zilizotengenezwa na
makampuni mengine zilizopo kwenye masoko hivi sasa na inao uwezo wa kudaka
mawasiliano na kusikika vizuri hata iwapo mtumiaji anasafiri kwa kutumia treni
iendayo kasi kwa mwendo wa kilometa 300 kwa saa.
0 comments:
Post a Comment