BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
imeongeza muda wa waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwasilisha
maombi yao hadi mwishoni mwa mwezi huu.
Taarifa iliyotolewa jana na HELSB nanakusainiwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa wake, George Nyatega, imesema hiyo ni kutoa fursa kwa wombaji ambao
hawajakamilisha kufanya hivyo.
“Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao
kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika muda
uliopangwa,” ilisema sehemu ya tarifa hiyo.
Awali Bodi ilianza kupokea maombi ya mikopo kupitia
mtandao wake wa kwa www.olas.heslb.go.tz tamngu mwanzoni mwa mwezi
Mei mwaka huu na mwisho wa maombi hayo ulipangwa kuwa Juni 30 mwaka huu.
Kupitia taarifa hiyo, HESLB imewataka waombaji wa mikopo
kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao hawajakamilisha maombi yao kukamilisha na
kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa na kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza
baada ya tarehe 31 Julai, 2015.
HESLB
ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi
Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji
waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu.
IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA
MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
0 comments:
Post a Comment