Meneja wa timu ya
Coastal Union,Akida Machai kushoto akimkabidhi Jezi ya Klabu ya Coastal
Union winga mpya wa Kulia,Ibrahim Twaha "Messi"mara baada ya kusaini
mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.
***********
NA MWANDISHI
WETU,TANGA
TIMU ya Coastal
Union ya Tanga imeendelea kufanya usajili wa nguvu ili kujiimarisha vilivyo katika safu mbalimbali
ambapo jana ilifanikiwa kuingia mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha
miaka miwili aliyekuwa winga wa kulia wa Simba,Ibrahim Twaha “Messi”
Utiliaji
saini wa mkataba huo ulifanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mjini hapa
na kushuhudiwa na viongozi waandamizi akiwemo Katibu Mkuu Kassim El Siagi na
Meneja wa timu hiyo,Akida Machai.
Akiuzngumza
mara baada ya kumalizika utiaji saini huo,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim
El Siagi alisema kuwa wameamua kumsajili mchezaji huyo kutokana na uwezo mkubwa
aliokuwa nao hasa anapokuwa uwanjani .
Alisema kuwa
winga huyo ana vitu adimu ambavyo akishirikiana na wachezaji wengine ambao
wamesajiliwa katika timu hiyo itakuwa chachu ya kuipa maendeleo timu hiyo
katika msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.
“Niseme tu safari hii tumedhamiria kuleta
mabadiliko makubwa kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara na hili
tunalifanya kuhakikisha tunarudisha kombe mkoani hapa ambalo tulilichukua mwaka
1988 “Alisema El Siagi.
Kwa upande
wake,Ibrahim Twaha “Messi”mara baada ya kusaini mkataba huo alihaidi kuipa
mafanikio timu hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine katika safari za
kuwania Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao.
“Sasa ni kama nimerudi nyumbani kwa sababu
awali nilikuwa naitumikia timu hii hivyo najisikia faraja kubwa kurudi tena
Coastal Union mi nihaidi kushirikiana nao kwa lengo la kuipa mafanikio “Alisema
Messi.
Awali
akizungumza,Meneja wa Coastal Union,Akida Machai alisema kuwa msimu huu timu
hiyo imedhamiri kufanya usajili nzuri ambao utaiwezesha kutwaa ubingwa na
kurudisha makali yao ya miaka ya nyuma.
0 comments:
Post a Comment