Wajumbe wa Kamati ya Media Car Wash for Cancer wakimkabidhi Adol Kivamwo mfano wa hundi wenye thamani ya shilingi Milioni 10 kwaajili ya kusaidia matibabu yake ya saratani. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam hii leo.
************
Waandishi wa habari watatu, Adolf Simon Kivamwo,
Athumani Hamisi na Danstan Bahai wamekabidhiwa jumla ya TZS 20m/- kwa ajili ya
kulipia gharama za matibabu yao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia
waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson alisema kuwa
fedha hizo ni matunda ya harambee ya Media
Car Wash for Cancer Campaign, inayoendelea nchini.
Kama tujuavyo, kwa kuanzia, wanahabari kutoka
vyombo mbalimbali Jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau wengine
waliosha magari kwenye viwanja wa Leader Club Julai 4, 2015.
Alisema katika harambee hiyo jumla ya 31m/-,
zilipatikana, ambapo kati ya fedha hizo, ndizo wagonjwa wamegawiwa.
“Malengo yetu ya awali yalikuwa kwamba tuwachangishe
fedha kwa ajili ya wenzetu wagonjwa, pia kiasi kingine kitumike kuwaingiza
baadhi ya wanahabari kwenye mifuko rasmi ya Bima ya Afya. Na ndivyo
tulivyofanya leo hii,” alisema.
Bw Thompson alisema kiasi kilichosalia kitatumika
kuwaingiza waandishi wa habari 100 katika mpango wa kulipia matibabu kupitia mfuko
wa Bima ya Afya, yaani NHIF.” Alisema.
Alisema lengo la harambee hiyo ni kukusanya jumla
ya 100m/- kabla ya mwezi Disemba 2015 na kazi yake kubwa itakuwa kuwahudumia
wanahabari wasiojiweza kwa sababu ya kusumbuliwa na maradhi mbalimbali.
Pia pesa zitokanazo na harambee hiyo zitasaidia
kuanzisha mkakati wa mkubwa wa kuhakikisha wanahabari wote nchini wanaingizwa
kwenye mfuko wa Bima ya Afya.
“Lengo letu ni kuhakikisha wanabari wana kinga za
afya zao,ili tukomeshhe huu mtindo wa kuchangiana mara kwa mara kila mmoja
anapougua,”alisema na kuongeza kuwa watakaohusika katika zoezi hilo, ni wale wasioajiriwa
pamoja na wasioajiriwa lakini hawana huduma ya Bima ya Afya.
Ili kuendeleza mchakakato wa kufikia lengo kuu,
wanahabari Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na wenzao wa Jijini Dar es Salaam,
Agost 15 mwaka huu, wataosha magari kwenye viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.
Tunaomba wadau mbalimbali waungane nasi kwenye
hili,ikiwemo kulipia gharama mbalimbali ukiwemo usafiri kwenda na kurudi
Mwanza,hoteli, matangazo ya radio na mabango.
Wakati huo huo Bw Thompson amesema kutakuwa
mkutano wa wadau habari Jumamosi Agost 1, mwaka huu utakaofanyika Msimbazi
Centre Jijini Dar es Salaam kwa jili ya kuanzisha mchakato wa usajili wa rasmi
wa kampeni hii.
“Tunaomba wanahabari wote nchini watakaoweza
kuhudhuria wasikose kufika, maana hapa ndipo juhudi za ukombozi wa kiafya kwa
wanahabari zitakapoanzishwa rasmi,” alisema.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo alisema kuwa Kamati yake
imewashirikisha wahariri wote nchini katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa
na kwamba viongozi hao wa vyumba vya habari ndio waliotoa majina hayo kwa
kamati.
Benjamin Andongolile Thompson
Mwenyekiti
Kamati ya Maandalizi
0 comments:
Post a Comment