MKUU wa wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Glorious Luoga, (Katikati), akinyanyua juu mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 800, baada ya kukabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampouni ya Acacia, Brad Gordon, (kushoto), katika hafla fupi iliyofanyika kwenye lango la kushukia kutyoka kilele cha Mlima Kilimanjaro, Mweka, Juni 28, 2015, Fedha hizo ambazo ni kwa ajili yab kusaidia sekta ya eli kwa watoto kutoka familia duni, zimetokana na wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki, kupanda Mlima Kilimanjaro kwa nia ya kuchangisha fedha chini ya mpango wa kampuni hiyo wa "CanEducate".
Brad, (kushoto), akikabidhi hundi hiyo kwa Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga
Brad, akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo, akiwa
Brad Gordon, (wakwanza kulia), akiongoza timu ya watu 21, wakiwemo wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki, kushuka Mlima Kilimanjaro wakitokea kileleni, kwenye lango la Mweka
Furaha baada ya kufanikiwa kufika Kilele cha Mlima Kilimanjaro na kurejea salama
Afisa Mtendaji Mkuu wa Acacia, Brad Gordon, (Katikati), Makamu wa Rais wa Acacia anayeshughulikia masuala ya kampuni, Deo Mwanyika, (wakwanza kulia), Meneja Mkuu wa uendelezaji wa kampuni ya Acacia, Asa Mwaipopo, (wapili kulia), Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga, (watatu kulia),wakiwa katika picha ya pamoja na watu 21 waliofanikiwa kupanda Mlima Kilimanjaro
Brad, akipongezana na Deo
Deo akitoa shukrani baada ya timu ya watu 21, walioongozwa na Brad, kufanikiwa kupanda na kurejea salama kutoka kilele cha mlima Kilimanjaro.
************
Kampuni
ya Uchimbaji Acacia, inayojishughulisha na uchimbaji na utafutaji madini, ,
imekusanya zaidi ya shilingi milioni 800 kupitia upandaji wa hisani wa mlima
Kilimanjaro ambao unalenga kuchangisha fedha za kusaidia sekta ya elimu nchini
chini ya mpango wa “CanEducate”, uliobuniwa na kampuni hiyo miaka mitano
iliyopita.
Timu
ya wafanyakazi, marafiki na wanafamilia wa Kampuni ya Acacia wapatao 21
wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Brad Gordon, wamerudi kutoka safari ya
kupanda mlima Kilimanjaro iliyowachukua siku sita.
Kupitia
mpango huo wa CanEducate, mpango
ambao unatoa ufadhili wa elimu kwa watoto wanaotoka familia duni, zinazoishi
maeneo yanayozunguka migodi inayomilikiwa na kampuni hiyo, ya North Mara,
Bulyanhulu na Buzwagi, Acacia imeanza utaratibu wa kila mwaka wa kualika
wafanyakazi, marafiki na wahisani kuchangisha fedha kwa njia hiyo ya upandaji
mlima.
Akizungumza
na wandishi wa habari kwenye lango la kushukia la Mweka, Afisa Mtendaji Mkuu wa
Acacia amesema ni jambo la kujivunia kuona kampuni imefikia lengo la kukusanya
kiwango cha dola 200,000, sawa na shilingi za Kitanzania Milioni 800, kupitia
zoezi hili, fedha ambazo zitakuwa na matokeo makubwa sana kwa kugusa maisha ya watoto wengi nchini
Tanzania.
“Tayari
tumekwisha fikia lengo la kukusanya dola 200,000 huku michango zaidi ikiendelea
kumiminika. Tunayaasa makampuni na watu binafsi kuendelea kuchangia kwani zoezi
lipo wazi hadi mwisho wa mwezi Julai,” alisema Brad.
Aidha,
ameongeza kuwa kwa kila dola moja itakayochangwa na wafadhili, pia Kampuni ya
Acacia itaongeza dola moja na hivyo kufanya jumla ya fedha zitakazoelekezwa
kusaidia sekta ya elimu kupitia mpango huu kufikia kiasi cha dola 400,000 kwa
mwaka huu.
Kwa
kuzingatia kuwa inagharimu kiasi cha dola 75 kwa mwaka kupeleka mwanafunzi
shuleni nchini Tanzania, fedha zilizokusanywa zina uwezo wa kusaidia wanafunzi
zaidi ya 2,000 wasioweza kumudu gharama za masomo hususani kutokea jamii jirani
na migodi ya Acacia yaani Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara iliyoko mkoani
Shinyanga na Mara.
Mpango
wa CanEducate ulianza mwaka 2010 kwa kuwanufaisha wanafunzi takribani 158 katika
maeneo ya Bulyanhulu na hadi mwisho wa mwaka 2014 mpango umekuwa hadi kufikia
kuwanufaisha wanafunzi zaidi ya 1,800 katika maeneo ya Bulyanhulu, Buzwagi na
North Mara na wanafunzi hawa wameonyesha ufaulu mzuri katika shule mbalimbali
katika mitihani yao ya Taifa.
Mlima
Kilimanjaro,, unatambulika kuwa mlima
mrefu zaidi barani Afrika nan i wa tatu duniani ambao kufikia kilele cha Uhuru mita
5,895 ni hatua ya juu barani Afrika. Kampuni ya Acacia ina mtazamo kuwa Elimu humfanya binadamu kuwa huru sababu
ambayo inaufanya mpango wa CanEducate kufaa kukusanya fedha kupitia kupanda mlima hadi kufikia
kilele cha Uhuru Peak.
Waweza
kuchangia Elimu kupitia upandaji mlima huu wa hisani, kupitia tovuti ifuatayo; http://caneducate.ca/kili-climb.html
0 comments:
Post a Comment