Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro (kushoto), akizungumza na viongozi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe, Wabia wa eneo la mradi wa Kampuni ya World Map na wawekezaji kutoka nchini China waliofika wilayani humo jana kuangalia fursa za kuwekeza viwanda katika eneo hilo. Kulia ni Ofisa Mipango Miji Mwandamizi kutoka TIC, Elibariki Ngorovily.
Wawekezaji kutoka China wakiwa katika mkutano na uongozi wa wilaya ya Kisarawe na wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map kabla ya kwenda kuona eneo la mradi wa viwanda. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Makampuni ya Huallan 'Huallan Group', Tu Huobao, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo, Apple Ye, Huang Haitao na Meneja Masoko, Nara Zhou.
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoko (kulia), akizungumza katika mkutano huo wakati akiwakaribisha wawekezaji hao. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro, Ofisa Mipango Miji Mwandamizi kutoka TIC, Elibariki Ngorovily, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Kigalu, Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Adam Ng'imba.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Adam Ng'imba (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoko na Mkuu wa Wilaya hiyo, Subira Kigalu.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Subira Kigalu akizungumza katika mkutano huo.
Wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map na viongozi wa idara mbalimbali za wilaya hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
Wakuu wa idara wa wilaya ya Kisarawe wakiwa kwenye
mkutano huo.
Mkutano na wawekezaji ukiendelea.
Maofisa wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map wakiwa kwenye mkutano huo.
Miundombinu ya barabara inavyoonekana eneo la mradi.
Katapila likiwa eneo la mradi kutendeneza miundombinu ya barabara.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro (katikati), akiwaonyesha ramani ya eneo la mradi wawekezaji hao. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Adam Ng'imba.
Mazungumzo eneo la mradi.
Sehemu ya eneo la mradi.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Subira Kigalu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji hao na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map.
***********
***********
Na Dotto Mwaibale
KATIKA kukuza uchumi kwa
wakazi Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani mradi wa uendelezaji wa
viwanja katika mji mdogo wa Kisarawe uliopo Kijiji cha visegese
umeanza kupata wawekezaji kutoka nchini China ili kusaidia kuendelea wilaya
hiyo kwa kujenga viwanda.
Wilaya hiyo kwa
kushirikiana na wabia kutoka kampuni ya world Map wameweza
kupima viwanja zaidi ya 250 katika kijiji hicho kwa ajili ya
viwanda na Kutangazwa katika maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi
na kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), na hatimaye kuanza kupata wawekezaji
ambao wametemebea katika wilaya hiyo na kujionea maeneo ya viwanda
hivyo.
Awali kabla ya kutembea katika
Kijiji cha visegese ambapo kuna viwanja ya maeneo ya uwekezaji mkuu
wa wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu ambaye ni mwenyeketi wa kamati ya
ulinzi na usalama wa wilaya hiyo aliwakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikisha
mazingira ya usalama kwa ajili uwekezaji
Akizungumza katika mkutano huo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoka
amekishukuru kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kuwaleta
wawekeza hao ili kufanikisha wananchi wa wilaya hiyo wanakuwa na uchumi wa kati
na kuongeza kodi kwa serikali.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu
wa TIC, Brendan Maro alisema wilaya hiyo imepiga hatua katika kutenga maeneo ya
viwanja kwa ajili ya uwekezaji hivyo kwa sasa kituo hicho hakinabudi kupeleka
wawekezaji katika maeneo ya pembezo.
Katika mradi huo wa viwanja
291 ambao asilimi 63 ni kwa ajili ya wananchi na asiliami 37 ni kwa ajili ya
halamshauri ya wilaya ya Kisarawe na wabia wa mnradi huo kwa
mafanikio hayo uwe ni chachu kwa halmashuri zingine ili kukuza uchumi kwa
wananchi kwa kutenga maeneo ya viwanda na kupima hali itakayosaidia kuepukana
na mipango miji holela.
0 comments:
Post a Comment