Katika jitihada za kuwafikia Watanzania
mbalimbali Benki ya Posta Tanzania (TPB) imezindua akaunti maalum kwa ajili ya
Vikundi Visivyo Rasmi. Uzinduzi huo ulifanywa na Katibu Mtendaji wa Shirika la Uwezeshaji Tanzania, Beng’i
Issa katika viwanja vya Shule ya Msingi Osterbay, Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa
Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi alisema, sasa makundi mbalimbali yasiyo
rasmi yanaweza kufungua akaunti na Benki ya Posta na kuweza kupatiwa mikopo ya
riba nafuu ya kuwawezesha katisha shughuli zao za ujasiriamali. ‘Tunaposema
akaunti za vikundi visivyo rasmi, ni vikundi kama vile jogging, vilabu mbalimbali
vya michezo, wasuka nywele, wasuka mikeka n.k., aliongeza Moshingi.
Makundi mengi yamejitokeza katika kufungua
akaunti hizi za vikundi visivyo rasmi, na hadi sasa akaunti takribani 340
zimefungulia kwa makundi yasiyo rasmi, alisema Moshingi. Kwa wiki benki
inafungua akaunti zaidi ya 16 kwa makundi haya, na tunapenda kuwahamasisha
makundi haya yajitokeze kwa wingi, ili waweze kunufaika na akaunti hii, alisema
Moshingi.
Kwa upande wake Beng’i Issa, alitoa pongezi kwa
Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kubuni akaunti hiyo maalum kwa makundi hayo.
‘Makundi mengi yanatamani sana, kupata huduma za kibenki kwa ajili ya shughuli
zao za kila siku, ila kutokana na uwezo sababu zilizo nje ya uwezo wao
wanashindwa kupata huduma hizo’, alisema Issa. Sasa makundi haya yajitokeze kwa
wingi katika kufungua akaunti hii Benki ya Posta iliwaweze kupata huduma
mbalimbali za kibenki ikiwemo, mikopo n.k aliongeza Issa.
Benki ya Posta Tanzania ni miongoni mwa mabenki
yanayokuwa kwa kasi nchini, ikifuata sera ya financial inclusion, yaani
kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za kifedha hapa nchini.
Benki hii hivi sasa ipo katika mchakato wa
kubadilisha sharia iliyoanzisha Benki ya Posta Tanzania, Sura ya 301, ili
kukidhi matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha na kanuni zake (The
Banking and Financial Institution Act, 2006 and its Regulations), ambayo
imeweka masharti kwa benki zote nchini kusajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni,
sura 212.
Mchakato huu wa kubadilisha sharia hiyo uko
Bungeni hivi sasa na uko katika hatua nzuri, na unalenga kuiwezesha Benki ya
Posta Tanzania kukidhi matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha na
Kanuni zake. Akizungumza mchakato huu, Moshingi alisema mara baada ya
kukamilika kwake, benki yake itaweza kujiimarisha zaidi na kuweza kutoa huduma
bora zaidi kwa wateja wake, katika wigo mpana zaidi.
Wajasiriamali, wakiwa wamekamata kadi ya ATM ya
benki ya Posta, baada ya benki hiyo kuzindua, huduma ya akaunti maalum kwa
vikundi visivyo rasmi, jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEEC), Beng’i Issa, (kushoto), akuzindua huduma maalum ya akaunti ya vikundi visivyo rasmi, Juni 24, 2015.
Katibu Mtendaji wa NEC, akizungumza wakayi wa uzinduzi huo
Maafisa wa juu wa benki hiyo, wakibadilishana mawazo wakati wa uzinduzi huo
0 comments:
Post a Comment