BAADA YA timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Star' kufanya vibaya katika mechi zake nyingi na kupelekea kuvunja benchi lake la ufundi lililokuwa chini ya kocha mholanzi
Mart Nooij, leo Rais wa TFF, Jamali Malinzi amemtangaza kocha msaidizi wa Yanga, mzaliwa wa Morogoro, Charles Boniface Mkwasa kushika nafasi hiyo.
Malinzi amesema Mkwasa atasaidiwa na kocha wa timu ya Mafunzo, Hemed Morocco, na kwapamoja watafanya kazi kwa kipindi cha miezi
mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania kufuzu kwa CHAN na
AFCON.
Uteuzi wa
makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na
leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine
duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha hao wazawa wamekidhi.
"Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho) alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa,” alisema Malinzi
Aidha Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.
Naye Mart Nooij aliyekua kocha
wa Taifa Stars, akiongea na waaandishi wa habari alisema anawashukuru
watanzania wote, serikali, wadau wa mpira wa miguu nchini na TFF kwa sapoti
waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa.
Nooij alisema alifurahia maisha yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote alichokua akifundisha timu ya Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho wa ajira yake hana jinsi anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka Tanzania na watanzania wote kila siku kwa ukarimu wao.
0 comments:
Post a Comment