Mratibu
wa Kipindi cha Diaspora,Maggid Mjengwa akizungumza na waandishi wa
habari juu ya kipindi cha Diaspora kitachoanza kuruka katika kituo cha
TBC hivi karibuni katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo,Kushoto ni
Mkurugenzi wa Diaspora Intiative,Emmanuel Mwachullah,Kulia ni Mkurugenzi
wa Idara ya Mambo ya Nje wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa,Rosemary Jairo.
****************
ATANZANIA walioko
Ughaibuni wanatakiwa kuelezwa vitu ambavyo vitawafanya watanzania
nchini kutambua umuhimu wa watu katika masuala mbalimbali ikiwemo
uchumi.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo
jijini ,Dar es Salaam,Mratibu wa Watu Waishio Ughaibuni
(Diaspora),Majjid Mjengwa amesema kutokana na kutambua uwepo watu
milioni mbili wako nje nchi ambao wanatakiwa kushirikishwa katika
masuala mbalilmbali yanayoendelea nchini.
Amesema
katika kipindi hicho kitatoa mwanga kwa watu wa ughaibuni na watanzania
nchini juu kushirikiana katika masuala mbalimbali.
Kwa
upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nchi na Ushirikiano wa
Kimataifa,Rosemary Jairo amesema kuwa ubunifu wa mjengwa wa kipindi cha
Diaspora kitasaidia kuelimisha watanzania juu maana wakishajua itakuwa
ni rahisi kupata uraia pacha.
Amesema
watanzania wengi hawajui faida ya kuwa na watu nje ya nchi katika
masuala ya uchumi wanawezaje kuchangia kuleta maendeleo.
Jairo amesema kuna watanzania wanafanya kazi ughaibuni wanafanya vizuri hali ambayo wanaweza kufanya katika nchi yao.
0 comments:
Post a Comment