Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (katikati) akiongea na waandishi wa
Habari leokatikaofisiza Airtel jijini Dar Es Salaam wakati wa uzinduzi wa ofakabambeitakayowazawadiawateja
wa Airtel nchinikupata Unit zabureza
LUKUpindiwatakaponunua LUKU kupitiahuduma ya Airtel Money, kushoto ni Afisa
uhusiano na matukio wa Airtel na (Kulia) Steven Kimea Meneja wa Airtel Money.
Meneja wa Airtel Money Steven Kimea (Kulia) akiongea na waandishi wa
Habari (hawapopichani)wakati wa uzinduzi wa ofakabambeitakayowazawadiawateja wa
Airtelnchinikujipatianyongeza ya Unit zabureza LUKUpindiwatakaponunua LUKU
kupitiahuduma ya Airtel Money,anayefwata kushotoni
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando.Hafla ya
uzinduzihuoimefanyikaleokatikaofisi ya Airtel jijini Dar es Salaam.
************
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana
na shirika la umeme la (TANESCO) imezindua ofa kabambe itakayowazawadia wateja
wake nchi nzima Unit za bure za Luku pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya
Airtel Money.
Ofa
hii mpya ina lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme na pia
kuwazawadia wateja wa Airtel wanaonunua unit za LUKU kupitia huduma ya Airtel
Money
Akiongea
kuhusu ofa hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackosn Mmbandoalisema” Wateja wetu
watazawadia unit LUKU za ziada Bure mara tu watakaponunua LUKU kupitia huduma
ya Airtel Money. Tunaamini ofa hii inaendana na mahitaji na mwendendo wa
maisha ya watanzania.
Kwa sasa manunuzi ya umeme kupitia njia nyingine si
tu yanaleta changamoto za kusafiri umbali mrefu na kupoteza muda mwingi
kupata huduma bali husababisha watu kukaa foleni ndefu kusubiri kununua umeme.
leo Airtel tunatoa ofa hii kwa wateja wetu na kuwawezesha kununua LUKU kwa
urahisi wakiwa majumbani mwao pamoja na kunawazawadia kwa kuwapatia unit za
Luku za ziada za bure”.
Aliongeza
kwa kusema “ Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu
zinazokithi na kutatua mahitaji ya wateja wetu , tukiwa na mawakala wa Airtel
Money zaidi ya 45,000 nchini , wateja wetu wanafaidika na huduma ya
mikopo, huduma za kuhamisha pesa, kutoa na kuweka pesa na nyingine
nyingi.
Huduma ya Airtel Timiza inayotoa mikopo isiyo na dhamana kupitia
simu za mkononi ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma za kisasa zenye
ubunifu kwa watanzania.” aliongeza Mmbando.
0 comments:
Post a Comment