Nafasi Ya Matangazo

June 24, 2015



Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akikabidhi hundi yenye dhamani ya sh.milioni 20  kwa Naibu katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Mohamed Khamis Said kwa lengo la  kusaidia futari kwa vituo mbalimbali vya watoto yatima hapa nchini wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
***************
Na Mwandishi wetu
Airtel Tanzania imetoa Tsh Milioni 20 kwa Jumuiya ya Waislamu kupitia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa lengo la kufuturisha vituo kumi vya kulelea watoto yatima nchini.

Akikabidhi hundi kwa Naibu katibu Mkuu wa Bakwata Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Hawa Bayumi alisema vituo vitakavyopata msaada huo ni pamoja na Kigogo Fresh orphanage cha Ilala, IHSANI orphanage cha Temeke,  Almadina center kinondoni.pia kwa Arusha ni Kiboa Islamic
orphanage, Nusuru yatima orphanage  Bukoba, Nuru orphanage Mbeya, Zam zam orphanage Dodoma, Maua Daftari Foundation Zanzibar,  Chuno orphanage center Mtwara  na Makorora Yatima center  cha Tanga ambapo kila kimoja kitapatiwa vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni2.

“Airtel Tanzania kama inavyofanya miaka mingine leo pia inaungana na ndugu na jamaa zetu waislamu kuadhimisha mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kwa kuwakumbuka watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia hivi vituo ili nao waweze kushiriki mfungo wa Ramadhan.” alisema.

Aliongeza kuwa Airtel imekuwa ikitoa misaada kama hii kwa makundi mbalimbali katika jamii kila mwaka na kusisitiza kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Airtel watajumuika na watoto hawa katika mwezi huu ili na wao pia wajiskie kama sehemu ya jamii.

“Tunapenda kutoa rai kwa mashirika mengine pia yawakumbuke hawa watoto na kuwasaidia ili wajisikie kama sehemu ya jamii,” alisema.

Akipokea hundi hiyo, Naibu katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Mohamed Khamis Said aliishukuru Airtel Tanzania kwa msaada huo na kusisitiza kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa na kuhakikisha watoto wanaolelewa katika vituo hivi wanapata mahitaji muhimu hasa katika mwezi huu wa
Ramadhan.

“Tunashukuru mno kwa niaba ya vituo hivi na tunatoa wito kwa mashirika mengine pia yajitokeze na kutuunga mkono ili tuweze kufikia yatima wengi zaidi na kuwapa faraja katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan” alisema.

Posted by MROKI On Wednesday, June 24, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo