Hafla
hiyo ilifana kwa kiwango cha hali ya juu na iliyomfanya Zari kulia
jukwaani kwa furaha kutokana na alivyopokelewa na watanzania huku
wakiita Wifi, Wifi!!, Kila aliyehudhuria katika hafla hiyo alionekana
akiwa amevalia mavazi meupe na mwenye furaha. Lakini pia hata mimi
pamoja na kwamba nilienda kuripoti matukio ya hafla hiyo ilibidi
nifuate utaratibu kwa kugonga vitu vyeupe kama wengine ili nisije
nikaharibu shughuli ya watu.
Nilifurahia sana hafla hiyo kama walivyofurahia mashabiki wengine wa
Diamond na nitamkubali siku zote kwa kazi yake nzuri anayoifanya
kimuziki akiiweka Tanzania juu katika ramani ya muziki Afrika na
Duniani “Viva Diamond, Viva Zari” Asanteni.
Ilikuwa Full Burudani kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Picha zaidi: FULLSHANGWE BLOG




0 comments:
Post a Comment