Balozi
wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk(kushoto)
akiwa katika swala iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika msikiti wa msikiti wa Alsahaba ulioko eneo la Morombo jijini Arusha,ambapo
aliwatembelea waumini hao na kutoa zawadi za tende.
**********
Waislamu
kote nchini wametakiwa kujiandaa vyema na mwezi mtukufu wa Ramadhani
unaotarajia kuanza hivi karibuni kwani kipindi hicho ni cha kufanya
matendo mema na kuisaidia jamii hasa wahitaji.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa taasisi ya Islamic Foundation Bader Marei jana
katika swala ya ijumaa iliyofanyika katika msikiti wa Alsahaba ulioko
eneo la Morombo jijini hapa na kuhudhiriwa na Balozi wa falme la
kiarabu nchini .
Bader
huyo amesema kuwa kipindi cha Ramadhani ni kipindi cha kujitazama na
kubadili mwenendo na kuwa watu wanaofaa katika jamii.
Akizungumza
kwa niaba ya Ugeni huo wa Ubalozi wa falme hizo za kiarabu amesema kuwa
ziara hiyo inalenga kuangalia changamoto za kijamii na kuangalia namna
ya kuzitatua ambapo wamezindua visima 34 vya maji katika wilaya ya
Ngorongoro.
Mbali
na shughuli hizo pia wamegawa msaada wa tende kwa waislamu wote
waliohudhuria katika swala hiyo ikiwa ni moja kati ya maandalizi ya
Mwenzi huo mtukukufu.
Baadhi ya waumini walioshiriki katika swala hiyo Issa
Tesha muuminI na Saidi Hamis muumini wameeleza kufurahishwa na ujio
huo mkubwa ambao unashirikiana na jamii ya waislamu katika masuala mbali
mbali ya kijamii na kidini.
“Tumefurahi
kupata msaada wa tende kipindi cha Ramadhani upatikanaji wa tende huwa
mgumu lakini sasa walau tuna tende tunashukuru sana “ Alisema Issa.Picha na Ferdinand
Shayo wa jamiiblog.
0 comments:
Post a Comment