Nafasi Ya Matangazo

May 14, 2015


Mwandishi wa Habari wa Star Tv na Redio Free Africa Mbeya, Fredy Bakalemwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Mtandao huu umepokea kwa masikitiko makubwa  taarifa za kifo cha mwanatasnia huyo wa Sahara Media Group na upo pamoja na wanahabari wote, familia yake na marafiki zake katika kuomboleza kifo chake.

Bakalemwa ameondoka huku tasni ya habari ikipita katika kipindi kigumu kinachohusisha juhudi, mbinu na njama za wazi za kukwaza Uhuru wa kupata habari.

Kwa mfano, Sheria ya Takwimu ya mwaka 2014 yenye nia ya kurasimisha kila matokeo ya utafiti wa taasisi mbalimbali au watu binafsi wakiwemo wasomi; itaathiri wepesi na haraka ya kukusanya taarifa hivyo kuua maana ya habari kitaaluma.

Sheria ya Makosa ya Mitandao ya mwaka 2015 inanyima fursa adhimu ya uandishi wa habari za uchunguzi; hivyo kubaki na fursa pekee ya kuchapisha taarifa na habari kwenye mitandao ya Intaneti.

Kwa mfano kashfa ya Vodacom ambayo ni kubwa kuliko kashafa ya EPA na ESCROW imebakia kusomwa Jamii Forums pekee kwa kuwa vyombo vingine vyote vya habari, ama vimekosa ujasiri au vimeathiriwa na uhusiano wa kibiashara kati yake na kampuni hiyo.

Muswada wa Sheria ya Huduma kwa Vyombo vya Habari unapokonya kazi za Baraza la Habari Tanzania (MCT): hivyo uhuru wa waandishi wa habari kujiongoza na kujitawala unakuwa shakani; na sasa suala la maadili linafanywa kuwa la kisheria badala ya usuluhishi.

Mwisho Muswada wa Haki ya Kupata Habari, unaompa kila mwananchi haki ya kudai habari kutoka kwa mtoa habari wakiwemo watawala umekwazwa na ukiritimba wa elimu na malipo; jambo ambalo litampa wakati mgumu mwandishi mwenye sifa ya elimu chini ya digrii na mwananchi wa kawaida kupata habari anayoitaka.

Bakalemwa umeondoka, lakini umeacha kundi kubwa nyuma yako; tunaahidi kukuwakilisha vyema katika kudai haki na uhuru wa kupata habari.

R.I.P BAKALEMWA.
Posted by MROKI On Thursday, May 14, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo