




Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine aliwakumbusha Mabalozi kuwathamini Watanzania waishio nje ya nchi, kuendelea kusaidia upatikanaji wa misaada ya maendeleo, masoko ya bidhaa za Tanzania, wawekezaji na teknolojia bora. 



Mhe. Rais Kikwete akiteta jambo na Waziri Membe kabla ya kuwahutubia Mabalozi
Waziri Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu, Balozi Mulamula huku Balozi Sefue akisikiliza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.


Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Sekretarieti ya Mkutano wa Nne wa Mabalozi
Mhe. Rais Kikwete akiongozana na Balozi Mulamula kuelekea eneo la kupata picha ya pamoja.


Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na Waziri Membe, Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Balozi Sefue, Balozi Mulamula, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Simba Yahya, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mhe. Mussa Zungu, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wote.

Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
0 comments:
Post a Comment