Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magazeti ya daily News, Sunday News, HabariLEO, HabariLEO Jumapili na Spotileo wakishiriki katika maandamano ya siku ya wafabnyakazi jijini Dar es Salaam leo.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kuwahamasisha wananchi wote kujitokeza
kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura ili kuweza kupiga kura ya
maoni na kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.
Hayo
yamedhihirika leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
Mei 1, 2015 zilizofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo
wizara mbali mbali ikiwemo taasisi binafsi zilibeba mabango yenye ujumbe
kuhamasisha wafanyakazi.
Mpaka sasa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura linaendelea vizuri katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara.
Wafanyajkazi wa Benki ya Posta Tanzania nao wakishiriki katika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani hii leo.
Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzinao walishiriki...
Wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) wakiwa katika maandamano kusherekea siku ya Wafanyakazi Duniani MEI MOSI huku wakiwa na bango lenye ujumbe wao mahususi kuwahamasisha wananchi kushiriki kujiandikisha na wapige kura kuchagua kiongozi bora.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya anga nao hawakuwa nyuma na mabango yao.
Wafanyakazi wa Ofsi ya Rais - Ikulu...
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege ya Air Tanzania...
Mabango mbalimbali yamebeba kaulimbiu juu ya kuhamasisha wafanyakazi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura km. Nikiripoti toka Uwanja wa Taifa wa Zamani (Picha na Christina Njovu).
0 comments:
Post a Comment