Makongoro Nyerere
Mtoto wa Muasisi wa Taifa la Tanzania, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarange Nyerere, Makongoro Nyerere anataraji kutangaza nia ya kuwania kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Juni mosi mwaka huu, kijijini Butiama, mkoani Mara.
Makongoro ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki ameweka hadharani hilo na kutoa mwaliko kwa watu wa kada mbalimbali wakiwepo wanahabari kuhudhuria mkutano wake huo utakao anza majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 6 mchana.
Endapo Makongoro atashinda kinyang'anyiro hicho ambacho hadi sasa ndani ya CCM kimeonesha kuwavuta wanasisa wengi akiepo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Mawaziri kadhaa wa seruikali ya sasa atakuwa miongoni mwa watoto wa marais wanayaongoza mataifa ya Afrika.
Miongoni mwa watoto wanaoongoza nchi za Afrika na baba zao waliwahi kuwa marais ni Rais Joseph Kabila wa Congo DRC aliyemrithi babayake Lauraa Kabila, Rais Uhuru Kenyata wa Kenya aliyefuata nyayo za babayake Mzee Jomo Kenyata na pia aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar, Amain Abeid Karume aliyefuata nyayo za Muasisi wa Muungano wa Tanzania na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume.
0 comments:
Post a Comment