Balozi Seif kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein akiufunga Mkutano wa Nne wa siku Tatu wa Mabalozi wa Tanzania uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Ramada Mjini Dar es Salaam.Baadhi ya Mabalozi wa Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani walioshiriki Mkutano wao wakifuatilia Hotuba ya Ufungaji wa Mkutano huo iliyosomwa na Balozi Seif kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. ASli Mohammed Shein.Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Tanzania Nchi mbali mbali Duniani mara baada ya kufunga Mkutano wao wa Nne ulifanyika Ramada Hoteli Jijini Dar es Salaam. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Bernard Membe, Katibu Mkuu Mpya wa Wizara hiyo Balozi Lebereta Mula mula na kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Mhadhi Juma Maalim. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Jamuhuri ya Watu wa China Balozi Abrahaman Nyimbo mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania Mjini Dar es salaam. Picha na – OMPR – ZNZ.
---
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein alisema Mabalozi wanayoiwakilisha Tanzania katika Mataifa tofauti Duniani wanapaswa kuitekeleza vilivyo Sera ya Mambo ya Nje inayolenga katika Diplomasia ya uchumi ambayo ndiyo muongozo wao katika utekelezaji wa jukumu lao la msingi.
Alisema Sera hiyo ni vyema ikatumika vizuri wakati huu ambao Taifa la Tanzania linatekeleza Dira ya kuelekea uchumi wa Kati na kati ifikapo mwaka 2020 kwa upande wa Zanzibar na Mwaka 2025 kwa Tanzania Bara.
Dr. Ali Mohammed Shein alisema hayo wakati akiufunga Mkutano wa Nne wa siku Tatu wa Mabalozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.
Alisema katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje yenye kuweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi Tanzania imepiga hatua kubwa vikiwemo Visiwa vya Zanzibar.
Dr. Shein alifahamisha kwamba matunda ya Sera hii yanadhihirisha wazi ukuaji wa sekta ya Utalii, miradi mengine ya kiuchumi ikiwemo pia ile mikubwa inayotekelezwa na wahisani kwa upande wa Zanzibar.
“ Mikakati mipya ya muda mfupi na mrefu mliowekeana katika Mkutano huu ni msingi mzuri kabisa kufuatana na mabadiliko ya uchumi yanayotokea Duniani na kufikia malengo ya Dira ya 2020 na 2025 “. Alisema Dr. Shein.
“ Nina hakika kuwa katika Mkutano huu mmeweza kuziba nyufa zote zilizojitokeza katika utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 inayolenga katika Diplomasia ya Uchumi ambayo ndio muongozo wetu katika utekelezaji wake na ni jukumu letu la msingi “. Alisisitiza Dr. Shein.
0 comments:
Post a Comment