Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa
marehemu John Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo
zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es
Salaam leo Mei 11, 2015. Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho
kwa mwili wa marehemu John Nyerere, wakati wa shughuli za
kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani,
jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015.
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati alipowasili
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo cha msiba wa marehemu John Nyerere
0 comments:
Post a Comment