Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameonekana akicheza mpira pamoja na
marafiki zake mjini Bujumbura licha ya mgogora wa kisiasa nchini mwake.
Rais Nkurunziza,alikuwa akisakata kabumbu ndani ya mji mkuu wa
Bujumbura mji uliokumbwa na maandamano makubwa tangu atangaze nia ya
kuwania awamu ya tatu uongozini.
Hii leo habari kutoka Burundi zinasema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Bujumbura.
Mtu huyo alikuwa miongoni mwa waandamanaji wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa awamu ya tatu.
Walioshuhudia
wanasema kuwa polisi walimpiga mwandamanaji huyo risasi mgongoni wakiwa
katika eneo la Musaga linalotazamwa kama ngome ya upinzani.
Waandamanaji walijaribu kufika katikati mwa jiji la Bujumbura lakini walitimuliwa kwa mabomu ya moshi wa kutoa machozi.
Rais
wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewaomba zaidi ya raia laki moja na
hamsini waliokimbia ghasia nchini humo katika majuma kadhaa yaliyopita,
warejee nyumbani. SOURCE: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment