Nafasi Ya Matangazo

October 16, 2026





Dar es salaam
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dennis Londo amewataka wafanyanyabiashara na wamiliki wa Viwanda kutoka nchini Uturuki Kutumia fursa ya kuanzisha Viwanda hapa nchini ili kunufaika na masoko ya Biashara ya Afrika, SADC na EAC

Waziri Londo ameyasema hayo Leo Wakati alipokutana na ujumbe wa rais wa Wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda kutoka nchini Uturuki ambao uko nchini Kwa ajili ya kuangalia fursa za kibiashara nchini Tanzania.

Amesema Tanzania inatamani uturuki kuwekeza Kwa wingi kwenye viwanda ili kuongeza tija Zaidi na Kuongeza kuwa, Tanzania imeweka Mazingira mazuri Kwa ajili ya wawekezaji wanaokuja kuwekeza hapa nchini.

‘’ ujumbe huu ni muhimu sana kwa nchi yetu kwani wafanyabiashara na wamiliki hawa wa viwanda wanachangia pato la Taifa la nchini Uturuki Kwa takribani asilimia 30’’ alisema Mhe Londo.

Awali akizungumza juu ya ujio wao,rais wa wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda kutoka Uturuki Bwana Abdullah Demir amesema, wako tayari kuwekeza kwenye bidhaa za viwandani Kama unga, vyakula vya samaki  na mifugo pamoja na kujenga kituo cha biashara hapa nchini.

Ujumbe huo wa wafanyabiashara  unatarajia kukutana na wadau wa Biashara na uwekezaji hapa nchini na  wale wa Zanzibar.
Posted by MROKI On Friday, October 16, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo