Nafasi Ya Matangazo

April 30, 2015


Mkurugenzi wa halmshauri ya wilaya ya Ruangwa, Nicholous Kombe (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 100 kwa Mwenyekiti wa WAALIMU SACCOS ya Ruangwa, Hamisi Malunga (kushoto)  ikiwa ni mkopo uliotolewa na mfuko wa pensheni wa LAPF kwa wanachama wa SACCOS hiyo. Katikati yao ni Meneja wa LAPF, Kanda ya mashariki, Yessaya Mwakifulefule pamoja na wanachama wa Saccos hiyo wakati wa mabidhiano hayo juzi Wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Wanachama wa  Walimu Saccos wa Wilaya  ya Ruangwa mkoani Lindi wakifurahia   mkopo wenye thamani ya shilingi Milioni 100 uliotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa wanachama wa Saccos hiyo. Anaeshuhudia wa pili kulia ni Meneja wa LAPF,  Kanda ya Mashariki, Yessaya Mwakifulefule. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika Wilayani Ruangwa hivi karibuni.
***************
Mfuko wa pensheni wa LAPF leo umetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni mia moja kwa Saccos ya waalimu iliyopo wilayani ruangwa mkoani Lindi.

Akipokea hundi ya mkopo huo kwa kwa niaba ya wanachama wa Waalimu Saccos,mkurugenzi wa halmshauri ya Ruangwa Bw Nicholous Kombe aliishukuru mfuko wa LAPF kwa kuwajali na kuwawezesha wanachama wa SACCOS hiyo ambao walikua wakiuhitaji sana mkopo wa aina hiyo.

Akishukuru kwa niaba ya waalimu wanachama wa saccos hiyo,Mwenyekiti wa saccos Bw Hamisi Malungu aliwaomba wanachama wake wadumishe nidhamu na kuheshimu kulipa mikopo yao kwa wakati ili Saccos yao iweze kukopesheka Zaidi.

Nae Meneja wa LAPF kanda ya mashariki Bw Yessaya Mwakifulefule,aliwapomgeza wanachama wa SACCOS hiyo na kuwashauri waalimu wengi Zaidi wachague kuchangia makato yao kwa mfuko wa LAPF ili na wao waweze kufaidika na mikopo kama hiyo li waweze kuwajikwamua kiuchumi.

Aidha bwana Mkwakifulefule alisema mpaka sasa LAPF imesha kopesha Zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa saccos mbali mbali za wanachama ambao makato yao wanachangia ktk mfuko huo hapa nnchini.

Waalimu SACCOS ilianzishwa mwaka 2001 ikiwa na wanachama 60 ambapo mpaka sasa saccos hiyo ina wanachama Zaidi ya 300 na hisa zenye thamani ya shilingi 26,000,000.
Posted by MROKI On Thursday, April 30, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo