Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha
Brigedia Jenerali Hashim Iddi Mbita (mstaafu) kilichotokea tarehe 26 Aprili 2015.
Brigedia Jenerali Hashim Mbita (mstaafu)
alizaliwa tarehe 02 Novemba 1933 katika mtaa wa Songoro, Kata ya Gongoni,
Wilaya ya Tabora Mjini, katika Mkoa wa Tabora.
Alisoma
shule ya Msingi ya Government Town Primary School Mkoani Tabora kuanzia mwaka
1946 hadi 1949. Alijiunga na Government Secondary School Tabora Mwaka 1950 hadi
alipohitimu kidato cha sita Mwaka 1957. Mwaka 1960 alijiunga na Chuo cha East
African School of Co-operatives kilichopo Nchini Kenya.
Marehemu
Brigedia Jenerali Hashim Mbita baada ya masomo yake alijiunga na JWTZ tarehe 01
Novemba, 1968 na kutunukiwa Kamisheni tarehe 26 Aprili, 1969.
Alistaafu
Utumishi Jeshini kwa Heshima tarehe 31 Desemba Katika utumishi wake marehemu
alishika Madaraka mbalimbali Ikiwemo Mkaguzi msaidizi Mkoa wa Mwanza mwaka 1958
hadi 1960, Afisa Habari Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1960 hadi 1962, Afisa
Habari Mkuu wa Serikali mwaka 1962 hadi 1965,
Mwandishi
wa Habari wa Rais mwaka 1965 hadi 1967, Katibu mwenezi wa TANU Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1967 hadi 1968, Mwalimu
wa Siasa Chuo cha Maafisa Monduli 1969 hadi 1970, Katibu Mtendaji wa OAU Kamati
ya Ukombozi mwaka 1972 hadi 1989 na Balozi wa Tanzania
Nchini Zimbabwe mwaka 2003 hadi 2006.
Marehemu
Brigedia Hashim Mbita ameacha mke na watoto.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 29 Aprili, 2015
kuanzia saa 1:30 hadi 5:00 asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na
mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, saa 10:00
jioini baada ya Sala ya adhuhuri.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI HASHIM IDDI MBITA (MSTAAFU) AMINA
0 comments:
Post a Comment