Machezaji wa vishale(Darts) wa
klabu ya Friedz ya Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam wakiwa wameshika kikombe
mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya mchezo huo
yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Friendz walizawadiwa
Kikombe na Pesa taslimu Shilingi 100,000/=.
*************
Na Mwandishi Wetu.
KLABU ya Friendz Wanaume yenye
makazi yake Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika
fainali za mashindano ya mchezo wa Vishale(Darts) Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar
es Salaam na hivyo kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi 100,000/=.
Nafasi ya pili katika
mashindano hayo ilichukuliwa na klabu ya Lugalo ambayo ilizawadiwa pia Kikombe
na pesa taslimu shilingi 60,000/=.
Upande wa Wanawake timu ya
Friendz yenye makazi yake palepale Tiptop Manzese ilitwaa ubingwa wa Taifa na
hivyo kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi 60,000/= wakati nafasi ya
pili Wanawake ilichukuliwa na klabu ya Kimanga ambao walizawadiwa kikombe na
pesa taslimu Shilingi 40,000/=.
Fainali za mashinadano ya
mwaka huu zilikuwa na mchezo wa mmoja mmoja(Singles) na wawili wawili (Doubles)
kwa Wanawake na Wanaume ambapo upande wa Doubles Wanaume, Jemes Mlai na
Sylivanus Sylivester wote wa Ibukoni klabu waliiibuka mabingwa na hivyo
kuzawadiwa Kikombe na Pesa Taslimu Shilingi 120,000/=, wakati nafasi ya pili
ilichukuliwa na klabu ya Jemes Enea na Nungwa Sadiloa wote wa Polisi Balax
ambao walizawadiwa Kikombe na Pesa taslimu Shilingi 80,000/=.
Upande wa doubles Wanawake
Subira Waziri na Happiness Modaha wote wa Klabu ya Ibukoni waliibuka mabingwa
na kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu shilingi 60,000/= wakati nafasi ya pili
ilichukuliwa na Fabiola Namajojo na Veronica Sule ambao walizawadiowa kikombe
na pesa taslimu Shilingi 40,000/=
Upande wa mchezaji mmoja
mmoja(Singles) Wanaume, Erry Boates kutoka klabu ya Lugalo alitwaa ubingwa na
kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi120,000/= wakati nafasi ya pili
ilichukuliwa na Jemes Enea kutoka Klabu ya Polisi Balax ambaye alizawadiwa
Kikombe na pesa taslimu 60,000/=.
Akizungumza wakati wa kutoa
zawadi aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo, Katibu Tawala wa Wilaya ya
Kinondoni, Selestine Onditi, aliwashukuru washiriki wote kwa moyo wa kujitoa
kushiriki mashindano ya Kitaifa kutoka katika mikoa mitano kwa kujitegemea na
pili aliwapongeza mabingwa waliofanikiwa na wale ambao hawakufanikiwa
wakajipange kwa mwaka ujao.
Nae mwenyekiti wa Chama cha
Vishale Taifa(TADA), Gesase Waigama aliwashukuru pia washiriki wote nakuwatakia
safari njema za kurudi majumbani kwao pamoja na maandalizi mema kwa
watakaoshiriki mashindano ya mchezo huo ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa
kufanyika hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment