Balozi
wa Tanzania nchini China, Mh Abdulrahman Shimbo akitoa mawaidha kwa waalikwa
katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania)
zilziofanyika Ubalozini mjini hapa. Mh Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi katika
hafla hiyo iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing (TZ-SUB).(
Balozi
wa Tanzania nchini China, Mh. Abdulrahman Shimbo (wa tatu kushoto) na mkewe
Mama Shimbo (wan ne kushoto), wakiwa na viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi
Watanzania Beijing (TZ-SUB) katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Mh Balozi
Shimbo alikuwa mgeni rasmi.
Balozi
wa Tanzania nchini China, Mh. Abdulrahman Shimbo (wa pili kushoto) na mkewe (wa
tatu kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya za Wanafunzi
Beijing kutoka nchi za Afrika Mashariki waliohudhuria sherehe za miaka 51 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizofanyika Ubalozini mjini
hapa. Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi.
Wanafunzi Wakitanzania Beijing pamoja na wageni mbalimbali katika picha yapamoja na mgeni rasmi, Balozi wa Tanzania nchini China, Abdurahman Shimbo (mwenye suti katikati) na mkewe, katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Beijing (TZ-SUB) na kufanyika Ubalozini mjini hapa.
Balozi wa Tanzania, China, Mh Abdulrahman Shimbo (wa nne kushoto) na mkewe Mama Shimbo (wa tano kushoto)katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Wanafunzi Watanzania kutoka vyuo mbalimbali mjini Beijing katika sherehe za miaka 51 ya Muungano Ubalozini. Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wanafunzi Beijing (TZ-SUB), Ireneus Kagashe (kulia) akitoa
utangulizi katika sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania)
zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Wa kwanza kushoto ni mgeni rasmi wa sherehe
hizo, Balozi wa Tanzania, China, Mh. Abdulrahman Shimbo, Mkewe Mama Shimbo na
Katibu wa Shirikisho la Jumuiya za Wanafunzi nchini China, Michael.
Familia
na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China katika picha ya pamoja
wakati wa sherehe za miaka 51 ya Muungano zilizofanyika Ubalozini mjini hapa.
Sherehe hizo ziliandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing (TZ-SUB).
Wa sita kutoka kushoto ni mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini China, Mh.
Abdulrahman Shimbo, kushoto kwake ni mkewe, Mama Shimbo
***********
Na Mwandishi wetu, Beijing
WATANZANIA wametakiwa kuliombea
Taifa amani na kuulinda Muungano kwa kuwa ndio njia pekee inayowaunganisha
wananchi na hata kujenga undugu kwa nchi za Afrika Mashariki.
Mwito huo ulitolewa na Balozi
wa Tanzania nchini hapa, Abdulrahman Shimbo, katika sherehe za miaka 51 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliopelekea kuzaliwa Tanzania. Sherehe hizo zilizoandaliwa
na Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing (TZ-SUB), zilifanyika Ubalozini,
mjini hapa.
Balozi Shimbo alisema waasisi
wa Muunganio, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na rais wa kwanza wa
Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume waliasisi suala hilo kwa kuwashirikisha
wananchi wa pande zote mbili na lengo likiwa kuiunganisha Afrika Mashariki.
Alisema Muungano umezalisha
nchi ya Tanzania ambayo pamoja na mambo mengi mema yaliopo, pia nchi nyingi
duniani ikiwamo China zimejipanga kuwekeza katika uchumi wa viwanda ambao kwa
muda mrefu umekuwa ukisuasua.
Katika hatua nyingine, Balozi
Shimbo aliwataka wananchi kutumia ardhi kama njia pekee ya kupambana na
biashara haramu ya dawa za kulevya, kwa kuitumia kuwekeza na kuwaajiri vijana
ili kulilinda Taifa dhidi ya kuangamia kwa nguvu kazi yake yaani vijana.
Balozi alisema ardhi iliyopo
nyumbani Tanzania, inatosha kuleta mapinduzi ya ajira kwa vijana nchini, na kuwataka
wananchi kuitumia kwa mujibu wa utaratibu uliopo, kupambana na biashara haramu
ya dawa za kulevya.
Mwito huo aliutoa kufuatia
igizo lililofanywa na TZ-SUB likibeba ujumbe wa “Tuungane kutokomeza dawa za
kulevya” ukienda sambamba na matukio ya kukamatwa kwa watanzania nchini China,
wengi wakiwa vijana wakijihusisha na biashara ya kusafirisha dawa hizo.
“Igizo ni ujumbe tosha, vijana na watu wazima
baadhi wanajidanganya kutafuta fedha isiyo halali, biashara hii ni ya dhambi na
inaharibu vizazi, vijana wengi hawawezi kutibiwa tena, fedha za dhambi
zinatisha,” alisisitiza Balozi Shimbo.
Sherehe hizo zilizoambatana na
burudani ya igizo na muziki, zilihudhuriwa pia na viongozi wa Wanafunzi
wanaosoma Beijing kutoka nchi za EAC ikiwamo Uganda, Rwanda na Burundi. Wakitoa
salamu zao, viongozi hao wa EAC waliisifu Tanzania kwa Muungano na kuomba udumu.
0 comments:
Post a Comment