Baaadhi ya mabango yaliyokutwa katika Karamu lililopo kijiji cha Nndatu wilayani Arumeru baada ya wananchi kuvamia shamaba hilo usiku wa manane na kuamua kuotesha migomba. |
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akiwa ameongozana na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo kutembelea eneo hilola Shamba akiungana mkono na hatua hiyo ya wananchi. |
ARUMERU.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha
Nkoaranga na Poli wameingia katika Shamba la Karamu (Karamu Estate)
usiku wa manane na kuamua kuotesha migomba kwa kile wanachodai
kuchoshwa na serikali kushindwa kusikia kilio chao cha kurudisha ardhi
ya mashamba makubwa yaliyomilikiwa na walowezi wakati wa
ukoloni.
Shamba hilo linalodaiwa kuwa na zaidi
ya Hekari 3500 lilivamiwa na wananchi hao na kuanza zoezi la kuotesha
migomba kabla ya kuning'iza mabango yenye ujumbe mbalimbali
katika maeneo tofauti ya shmaba hilo.
Wakizungumza kwa sharti la kutotaja
majina yao,wananchi hao walisema mashamba hayo enzi za ukoloni
yalipelekea Wananchi wa Meru kuchangia fedha kwenye Vyungu na kwamba
mwaka 1952 alitumwa marehemu Shujaa Japhet Kirilo kwenda umoja a
mataifa (UNO)kudai ardhi hiyo.
"Mwaka 1952 tulimtuma Shujaa wetu
Kirilo kwenda umoja wa mataifa (UNO) huko New York nchini Marekani
kwenda kudai ardhi hii ya wana Meru lakini hadi leo hii mwaka
2015 maeneo mengi hayajarudi mikononi mwa wazawa."alisema mmoja wa
wananchi hao.
Akizungumzia hatua hiyo Mbunge wa
Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari alisema amejaribu kupiga
kelele Bungeni huku akisaidiwa na waziri kivuli wa Ardhi ,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi ,Halima Mdee lakini bado kelele zao
hazijasikika.
"Binafsi nikisaidiwa na Halima
Mdee,Waziri Kivuli wa Ardhi,tumepiga kelel vya kutosha Bungeni
,serukali sikivu bado haijasikia kelele zetu,Pengine sasa Waziri
Lukuvi na serikali hii ya CCM itasikia kilio cha wananci hawa
walioamua kuingia shambani na kuotesha Migomba"alisema
Nassari.
Alisema Shamba la Karamu lilikuwa
likitumika kwa kilimo cha Kahawa na kwamba kwa sasa limegeuka pori
huku mwekezaji akidaiwa kuuza kuni kwa wenyeji na kukodishiwa kulima
bustani ndogo ndogo za mboga.
Nassari alidai kuwa hivi karibuni
mwekezaji alidaiwa kumega eneo la shamba hilo na kisha kuliuza kwa
chuo kikuu cha Tumaini ,tawi la Makumira na kwa baadhi ya wageni
kutokana na kile kinachodaiwa kumalizika kwa muda wa umiliki wa miaka
99.
0 comments:
Post a Comment