Nafasi Ya Matangazo

March 31, 2015

Muasisi wa chama cha Tanzania Peoples Party na aliyendika chapisho la mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi  Dr. Aleck Che-Mponda, amefariki dunia leo.

Kwa mujibu wa mtoto wake Chemi Chemponda, baba yake amefariki akiwa anapata matibabu katika hospitali ya Masanna iliyopo nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.

Dr Che-Mponda alifanya utafiti muhimu kuhusu mgogoro katika ya Malawi na Tanzania kuhusu Ziwa Nyasa mwaka 1971 kwa ajili ya Ph.D yake kutoka Chuo Kikuu cha Howard (Howard University). Dissertation inaitwa, ''The Malawi-Tanzania Border and Territorial Disputes, 1968: A case study of Boundary and Territorial Imperatives in the new Africa". Dr. Che-Mponda alimkabidhi Mh. Balozi Manongi, nakala la andiko (dissertation) lake.  Kwa wasiofahamu, Dr. Che-Mponda ni baba yangu mzazi.


Posted by MROKI On Tuesday, March 31, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo