Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania mstaafu . Jenerari Mrisho Sarakikya akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokutana naye baada ya kutembelea kata ya Sing'isi na kusaslimiana na wananchi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha yenye lengo la Kukagua Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, inayotekelezwa na serikali kwa pamoja na wananchi huku akihamasisha uhai wa chama cha Mapinduzi , Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Naye Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mbunguni amewaambia wananchi katika mkutano huo amemshutumu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu kwa kutosikiliza ushauri alioutoa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa wilayani Loliondo na Ngorongoro kwa mawaziri ambao wizara zao zinahusika moja kwa moja katika maamuzi na kushughulikia matatizo ya migogoro ya Ardhi mkoani Arusha ambapo kumekuwa na migogoro karibu wilaya zote, kati ya mbuga za wanyama na vijiji ama kati ya vijiji na vijiji.
Nape amesema wakati waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akiitikia na kupokea ushauri huo na kuhamishia shughuli zake mkoani Arusha ambapo kwa sasa yuko mkoani humo akikutana na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi ili kutatua migogoro hiyo, Nyalandu amekaa kimya anaendelea na mambo yake.
CCM ndiyo yenye mkataba na wananchi kwani ndiyo iliyoomba kura kwa wananchi na Mh Waziri Nyalandu ana mkataba na CCM ambayo imempa kazi ili afanye kazi na kutatua matatizo ya wananchi, CCM haiwezi kukubali mambo yaiharibike kwa watendaji wa serikali kutowajibika kwa wananchi kwani ndiyo itakayoadhibiwa na wananchi wakati wa uchaguzi ujao, "Hivyo Nyalandu anatakiwa kufanya kazi ambayo CCM imempa na si kutafuta watu wa kumtetea si sawa" Amesema Nape Nnauye.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania mstaafu . Jenerari Mrisho Sarakikya akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Mh. Ole Nangole katikati ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na wananchi huku wakiwa na ndoo za maji na matawi ya miti wakati alipofika katika kijiji cha Kimundo kata ya Nkoarisambu ambao wananchi wanachimba mawe na kubadilishana na maji kutokana na shida ya maji. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na askofu wa Meru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribishwa na wananchi wakati alipotembelea Patandi mahali aliposoma. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya uanachama wa CCM aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Monduli Bw. Amani Ole Silanga. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na wananchi kwa matawi ya miti mara baada ya kumpokea katika kijiji cha Sing'isi. Baadhi ya mashine za kuvuna mpunga kwa ajili ya wakulima wa mpunga USA River Lekitatu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la mashine za kukoboa na kufungasha mpunga USA River Lekitatu. Mkuu wa wilaya ya Arumeru Bi. Husna Mwilima akizungumza na wananchi wakati akielezea mkakati wa serikali ili kutatuo mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Maweni; Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Maktaba ya Ardhi MKURAVITA katika kijiji cha Mawezi.
0 comments:
Post a Comment