Nafasi Ya Matangazo

March 23, 2015


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na mmoja wa wanufaika wa mkopo kwa akina mama na vijana uliotolewa kwenye Kata zote za Manispaa hiyo, Victoria Mboweto alipotembelea mradi wake wa duka la nguo, Kigogo Mbuyumi, Dar es Salaam juzi. Manispaa hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya akina mama na vijana katika Kata zake

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na mmoja wa wanufaika wa mkopo kwa akina mama na vijana uliotolewa na Manispaa hiyo kwa Kata zote, Semeni Mahita ambaye ana mradi wa kuuza vitafunwa na mbogamboga sokoni alipotembelea mradi wake Kigogo Mbuyumi, Dar es Salaam juzi. Manispaa hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya akina mama na vijana katika Kata zake. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana wa Manispaa hiyo, Mwajuma Magwiza.

 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na mmoja wa wanufaika wa mkopo kwa akina mama na vijana uliotolewa na Manispaa hiyo kwa Kata zote, Semeni Mahita ambaye ana mradi wa kuuza vitafunwa na mbogamboga sokoni alipotembelea mradi wake Kigogo Mbuyumi, Dar es Salaam juzi. Manispaa hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya akina mama na vijana katika Kata zake. Kushoto ni mmoja wa wateja wa mwanamama huyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto) akinunua vikoi vya mmoja wa wanufaika wa fedha za mkopo za akinamama na vijana wa Manispaa hiyo, Thresia Mazwazwa (kulia) alipotembelea mradi wake, Sinza, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kwa ajili ya ukaguzi. Manispaa hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya akina mama na vijana katika Kata zake.
***********



NA MWANDISHI WETU, DSM
Manispaa ya Kinondoni imeahidi kuendelea kuwasaidia wakazi wake kwa kuwapatia mkopo wa vikundi kwa ajili ya kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda alisema kwa sasa Manispaa hiyo inaangalia uwezekano wa kuongeza kiwango cha mkopo kutoka shilingi milioni 500 mpaka kufikia bilioni 3.4 kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo zikiwemo taasisi za kifedha hususan benki ili walengwa waweze kunufaika na mikopo hiyo kwa riba nafuu.

Mwenda alisema kwa sasa Manispaa hiyo imetenga shilingi milioni 500 ambazo zimeelekezwa kukopeshwa vikundi vya akina mama na vijana katika Kata zote za Manispaa ambazo tayari zimeshakopeshwa kwa vikundi hivyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi yao.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa vikundi hivyo katika Kata za Kigogo, Sinza na Magomeni, mwishoni mwa wiki, Meya Mwenda aliwataka wanufaika wa mkopo huo kuendeleza miradi yao kwa ufanisi ili waweze kurejesha mikopo hiyo ambayo itasaidia kuwapatia wengine wenye uhitaji ili waweze kuendesha maisha yao na kujikwamua katika lindi la umasikini.

"Nataka kuona Manispaa yangu inakuwa mfano bora wa kuigwa kwa kutimiza malengo ya Serikali ya kuwapatia maisha bora wananchi wake kwa vitendo. Na sasa tumeanza kuwakopesha wananchi wa Manispaa yangu fedha hizi ambazo ni shilingi milioni 500 na kila Kata inufaike na mkopo huu wa riba nafuu. 

Wito wangu kwa wananchi wa Manipsa hii, ni kwamba Serikali yao inakopesha fedha hizi na watu waunde vikundi vyao ili waweze kupata mikopo hii. Wale wanaokaa tu wakilalamika Serikali haiwasaidii waachane na dhana hiyo, fedha hizi zipo wanaweza kusaidiwa. Hakuna Serikali itakuletea fedha nyumbani kwako, mjiunge kwenye vikundi kupitia Kata zenu. Serikali inachofanya ni kuweka mazu=ingira mazuri." Alisema.

kwa upande wao, wanufaika wa mkopo huo walimshukuru Meya huyo na kuiomba Manispaa iongeze fedha za mkopo kwani wengi wao wanaangalia kufanya biashara kubwa zinazohitaji mitaji mikubwa.
Posted by MROKI On Monday, March 23, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo