Mbunnge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akimkaribisha mratibu wa msafara wa wachungaji mbalimbali wa Makanisa ya Pentekoste kutomaeneo mbalimbali nchini, Mchungaji Bernedict Kamzee kutoka kanisa la Glory of Crist la mkoani Katavi.
Akizungumza Mchungaji Benedickto Kamzee, kutoka Kanisa la Glory
of Christ la Katavi, alisema wamefikia uamuzi huo wa kuja Dodoma kuonana na Edward Lowassa bila kushinikizwa wala
kushawishiwa na mtu yeyote.
“Hakuna
aliyetushawishi, hata siyo maaskofu wetu, hili suala halina msukumo wowote
zaidi ya msukumo wa Mungu,” alisema Kamzee.
Kamzee
alisema wachungaji hao wanatoka kwenye madhehebu ya EAGT, TAG, PEFA, KLPT
kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akizungumza na ujumbe huo wa Wachungaji waliofika nyumbani kwake pamoja na mambo mkengine ni kumuombea baraka za Mungu katika safari yake ya matumaini.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Khamis Mgeja akizungumza jambo wakati kuwapokea wageni hao.
Wachungaji hao wakiwa nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli mjini Dodoma.
Maombi yalifanyika na Mchungaji Bernedict Kamzee aliwaongoza wachungaji wote katika maombi hayo.
Maombi yakiendelea
Lowassa akiagana na wachungaji hao leo.
0 comments:
Post a Comment