Basi lenye namba za usajili T. 197 Scania mali ya kampuni ya OSAKA likiwa limepinduka baada ya kugonga tela lililokuwa limeharibika njiani.
Mnamo tarehe 13/03/2015 majira ya saa
23:34hrs huko barabara kuu ya Diodoma/Morogoro eneo la Chuo cha Biashara (CBE) Kata
ya Makole Manispaa ya Dodoma kwenye makutano ya barabara maarufu kama kona ya Dodoma
Inn, gari lenye namba za usajili T. 197 BUS Scania bus mali ya kampuni ya OSAKA
likiwa na abiria 57 likiendeshwa na Dereva SAID CHAUPENDO MSHANA mwenye miaka
33, Mkazi wa Dar es Salaam likitokea Bukoba kwenda Dar es Salaam, liligonga tela
lenye namba za usajili T. 533 BNM la gari lenye namba za usajili T. 426 BMJ
Scania lililokuwa likiendeshwa na IDD JUMA mwenye miaka 41, Mkazi wa Njedengwa Manspaa
ya Dodoma lililokuwalimeharibika.
Basi la OSAKA baada ya kushusha abiria
stendi kuu ya mabasi Dodoma liliondoka stendi likiwa katika mwendokasi na kushindwa
kusimama pamoja na kusimamishwa na Askari wa usalama barabarani waliokuwa kwenye
eneo ambalo tela lilipoharibikia. Kutokana na mwendokasi aliligonga
tela kisha kutumbukia mtaroni pembeni mwa barabara katika uzio wa chuo
cha Biashara (CBE) na kusababisha majeruhi kwa abiria mmoja aliyefahamika kwa jina
la JUSTA TRAZIAS mwenye miaka 19, Mkazi wa Ubungo River side Dare es Salaam
ambaye amelazwa katika hospitali ya rufaa Dodoma kwa matibabu na hali yake inaendelea
vizuri. Dereva wa basi hilo amekamatwa na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta
kondakta wa basi hilo.
Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva,
mwendokasi na kukataa kutii amri ya Askari aliposimamishwa kisha kushindwa kulimudu
gari na kusababisha ajali hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP ametoa wito kwa madereva
kuwa na udereva wa kujihami na wenye kuchukua tahadhari. Pia abiria waone umuhimu
wa kutoa taarifa pale wanapoona dereva anaendesha mwendokasi na kutotii sharia
za usalama barabarani mfano dreva huyu pamoja na kuwa mwendokasi pia inaonyesha alikuwa anakiuka maelekezo ya mabasi
kutotembea baada ya saa sita usiku kwani kwa muda huo alitakiwa walale stendi ya
mabasi Dodoma na ndiyo maana aliposimamishwa na Askaria likataa kusimama na
matokeo yake akasababisha ajali hii.
0 comments:
Post a Comment