Miongoni mwa manusura 22 wa ajali ya basi la Majinja lenye namba za usajili T438 CED wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa Iringa kwa matibabu. Abiria 42 walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Barabarani mkoa wa Iringa, Salim Asas Abri (kulia) akiwa na viongozi wengine wakiwajulia hali manusura wa ajali hiyo.
Kontena lilokuwa limepajkiwa katika lori la mizigo Scania
namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company likiwa limelalia juu ya basi lenye namba
za usajili T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja na kusababisha vifo vya watu 42
na wengine kadhaa kujeruhiwa jana katika eneo la Changarawe, nje kidogo ya mji
wa Mafinga mkoani Iringa leo.
Foleni ya magari katika eneo la Changarawe baada ya ajali hiyo.
Mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza (wa
pili kulia) akiwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi ,Mwenyekiti
wakamati ya Usalama Barabarani mkoa wa
Iringa Salim Asas Abri (wapili kushoto) na Mkuu wa Wilaya
ya Mufindi, Mboni Mhita eneo la ajali.
********
MAJINA YALIYOPATIKANA HADI SASA NI: Baraka
Ndone (dereva), Yahya Hassan ( kondakta), Ester Emanuel, Lusekelo
Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Teresia
Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana,
Catherine Mwate, Mwajengo, Ndulile Kasambala, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala,
Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule
na Dominick Mashauri, Omega Mwakasege.
Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick
Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi,
Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa
Iman Mahenge , Juma Sindu, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule,
Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo
wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na
Oswald.
Basi hilo lilianza safari mjini Mbeya likiwa na abiria 37.
0 comments:
Post a Comment