Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa(katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo juu ya hali ya urejeshaji mikopo ya wanafunzi. Kushoto ni Mkurugenzi Urejeshaji wa Mikopo wa HESLB, Juma Chagonja na Afisa habari, mwandamizi, Elimu na Mawasiliano, Veneranda Malima.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa(katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo juu ya hali ya urejeshaji mikopo ya wanafunzi. Kushoto ni Mkurugenzi Urejeshaji wa Mikopo wa HESLB, Juma Chagonja
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa(katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo juu ya hali ya urejeshaji mikopo ya wanafunzi. Kushoto ni Mkurugenzi Urejeshaji wa Mikopo wa HESLB, Juma Chagonja na Afisa habari, mwandamizi, Elimu na Mawasiliano, Veneranda Malima.
*******
IMANI potofu kuwa mikopo itolewayo
na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), ni ruzuku na hawapaswi kuirejesha ni moja ya
changamoto ambazo bodi hiyo inakabiliana nazo katika ukusanyaji wa madeni
kutoka kwa wanufaika.
Wakizungumza katika mutano na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo maofisa kutoka HESLB wamesema
makusanyo yamekuwa yakisua sua kutokana na wakopaji kutofanya marejesho na
kukaa kimya hata wanapo andikiwa.
Mkurugenzi wa Habari, Elimu na
Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, amesema kuwa jumla ya shilingi
Bilioni 123.8 zilipaswa kuwa zimerejeshwa lakini hadi sasa bodi imekusanya
Bilioni 65.2 pekee.
Bodi ya mikopo imekopesha wanafunzi
kiasi cha shilingi Trilioni 1.8 tangu mwaka wa masomo 1994/95 hadi Juni mwaka 2014
kati ya fedha hizo bilioni 51 zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi
na Teknolojia.
Mwaisobwa alisema
jumla ya wadaiwa 136,198 sawa na asilimia 76.94 ya wadaiwa wote 177,017 ambao
mikopo yao imeiva wametambuliwa na wanaendelea na marejesho ya mikopo.
“Hadi sasa mikopo
yote inayotolewa na Bodi kuanzia mwaka wa masomo 1994/95 inabeba tozo la
utunzaji wa thamani ya mikopo kwa asilimia sita kwa mwaka kwa kiasi chote cha
mkopo ambacho hakijarejeshwa” alisema.
Alisema bodi hiyo
inaendelea kuongeza kasi ya urejeshaji wa mikopo kwa kubuni mikakati mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kurejesha mikopo na
kuongeza matumizi ya mitandao ya simu katika kukusanya madeni.
Aidha njia mbadala
za utumiaji wa huduma za kifedha za mitandao ya simu kama M Pesa na Airtel
Money nazo zimeanza kutumika ili kuwarahisishia wakopaji namna ya kurejesha
fedha hizo badala ya kwenda kupanga folebni benki.
Pia alisema
wamezidisha ushirikiano zaidi na wadau muhimu hasa Mifuko ya Hifadhi ya Jamiii,
Mamlaka ya Mapato, Waajiri, Sekta isiyo rasmina Wanufaika wa mikopo ambapo pia
wamechukua hatua za kisheria dhidi ya wanufaika wanaokaidi kurejesha mikopo yao
ambapo hadi sasa kuna kesi 18 zimefunguliwa mahakamani dhidi ya wadaiwa sugu.
0 comments:
Post a Comment