Ujumbe wa Waziri wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi umemaliza ziara yake nchini Singapore huku ukiwa umejifunza mambo muhimu ikiwemo kuwepo utawala wa sheria katika usimamizi wa ardhi, kutokuwepo rushwa, nidhamu na uaminifu mkubwa wa watumishi wa umma, jamii inayopenda kujitegemea na usalama wa hali ya juu. Yafuatayo ni matukio ya ziara hiyo kwenye Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji wa Singapore(URA) kama yalivyoratibiwa na Muungano Saguya.
Ujumbe wa NHC ulipokutana na baadhi ya wawekezaji wakubwa wa sekta ya uendelezaji Miliki wa Singapore ili kuwahamasisha kuwekeza vitega uchumi vya hoteli nchini Tanzania. Ujumbe huu umekutana na Bw. Henry Ngo ambaye ni Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bonvest na Hoteli ya Sheraton Singapore ambao pia wamewekeza Zanzibar Hoteli ya Kitalii.
February 18, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment