Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene,
akikagua sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati
wa ziara aliyoifanya mwanzoni mwa wiki mkoani humo.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
(kulia) akijadili jambo na mmoja wa wasimamizi wa Mtambo wa kuchakata gesi wa
Madimba – Mtwara, wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua maendeleo ya
Mradi.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata
gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Luvula, Msimbati mkoani Mtwara, Yusuf Haki Yusuf (Kulia)
akiwasilisha maombi ya wananchi wa Kijiji chake kupatiwa umeme kwa
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kushoto)
wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki. Waziri aliahidi kuwa Kijiji
hicho na vingine 15 vilivyo jirani na MnaziBay vitapatiwa umeme kabla ya
mwezi Oktoba mwaka huu. Kulia kwa Waziri, ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,
Halima Dendegu.
*********
Na Veronica Simba
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene amefanya ziara mkoani Lindi na Mtwara
mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara yake ambapo
aliahidi huduma za umeme na maji kwa wananchi mbalimbali.
Akiwa
Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa
mtambo wa kuchakata gesi, Waziri Simbachawene alimwagiza Msimamizi Mkuu wa
Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba kutoa huduma ya maji safi kwa
wananchi wanaozunguka maeneo hayo.
“Kutokana
na taarifa yenu, mtakuwa na hifadhi ya maji ya kutosha hapa. Pamoja na matumizi
yenu mbalimbali, hakikisheni mnatoa huduma ya maji kwa wananchi wanaozunguka
mtambo,” alisema Waziri.
Vilevile,
Waziri Simbachawene alitoa ahadi ya umeme kwa Kijiji cha Luvula kilichoko
Msimbati. Alisema Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na Kiwanda cha
kufua umeme cha Mnazibay, vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
“Tunaendelea
na zoezi la kusambaza umeme nchi nzima. Lengo letu ni kuhakikisha idadi ya
watanzania wanaopata umeme inaongezeka zaidi na zaidi ili kuwezesha lengo la
nchi yetu kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama dira ya
maendeleo inavyoonesha,” alisema.
Ziara
hiyo ya Waziri Simbachawene, ni ya kwanza kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara tangu
aliposhika wadhifa wa Uwaziri wa Nishati na Madini, Januari mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment