Nafasi Ya Matangazo

February 11, 2015



 Mbunge wa viti maalumu Chadema, Chiku Abwao akikagua jengo lilokumbwa na ajali ya moto katika shule ya Sekondari Idodi.
Akiangalia moja ya mali za wanafunzi zilizoharibika na moto.
Mbunge wa Viti Maalum- CHADEMA, mkoa wa Iringa, Chiku Abwao ametembelea na kujionea athari zilizotokana na moto uliotekezeza bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Idodi mkoani humo.

Abwao alitoa pole kwa uongozi wa shule, wanafunzi na wazazi kufuatia ajali hiyo ya moto na kuwapa pole ya shilingi Milioni moja kusaidia waathirika.

Akizungumza mbele ya wanafunzi wa shule   Chiku Abwao amesema kuwa ameguswa na ajali hiyo ya moto ndio maana ameamua kujitolea kutoa msaada huo.

Aidha ameishauri serikali kujenga mabweni kwa mtindo nyumba za kawaida ili kuwawezesha  wanafunzi kuishi walau watoto 10 katika bweni moja tofauti na 

Pia amesema ipo haja ya kuwekwa ulinzi mzuri kwenye mabweni kwa kuwa suala kama hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika shule hiyo na kuomba wakandarasi watakao kuwa wanapewa tenda za kujenga mabweni ya shule kuhakikisha wanaweka vifaa maalum vya kuzimia moto.
Posted by MROKI On Wednesday, February 11, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo